HITILAFU ya kiufundi ambayo imesababisha kivuko cha Mv Magogoni kusitisha huduma kwa muda ya kuvusha watu kati ya feri ya Magogoni na Kigamboni jijini Dar es Salaam leo imezua bugudha na adha kubwa kwa wakazi wa pande hizo mbili waliokuwa wakielekea kazini na mashuleni.
Watu hao waliokuwa wakivuka kwa shida kwa kutumia kivuko kimoja baada ya Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) kukisimamsha kwa muda kwaajili ya matengenezo na kuwasihi wakazi waishio na kufanya kazi Kigamboni wanaotumia kivuko cha MV Magogoni kuwa wavumilivu
wakati kivuko hicho kikiwa kwenye matengezo ya hayo ya kawaida.
Akitoa ufafanuzi huo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Temesa, Marcellin Magesa
amesema, kivuko hicho kinafanya kazi saa 24 kwa siku, hivyo ili kifanye kazi vizuri kinahitaji matengenezo.
Amesema kivuko hicho kinalazimika kufanyiwa
marekebisho ya mara kwa mara ili kuhakikisha kinadumu kwa muda mrefu na kutoa
huduma kwa wateja.
Alisema matengezo hayo yatakamilika muda wowote na
kitaendela kufanya kazi kwani hakiwezi kutengzwa wakati wa usiku kutokana na
kufanya kazi muda wote.
Wananchi wakishuka huku wengine wakipanda katika kivuko cha Mv Kigamboni.
Wananchi waliokuwa wakisubiri kuingia katika MV. Kigamboni huku wakiwa na Baiskeli zao ambapo kwa wenye Magari wameambiwa wapite Darajani au mwenyekuweza apaki avuke.
MV. Kigamboni ikiwa inshusha upande wa Kigamboni
Taswira katika muonekano wa MV. Magogoni (kulia) ambayo ipo katika matengenezo na MV. Kigamboni
0 comments:
Post a Comment