Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa
na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Jumapili kinatarajiwa kucheza
mchezo wa kirafiki na timu ya University of Pretoria (Tucks FC) jijin
Johannesuburg ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Algeria
Novemba 14, mwaka huu jijini Dar es salaam.
Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya progamu ya kocha mkuu, Charles
Mkwasa baada ya kufanya mazoezi na vijana wake kwa takribani siku nne
mpaka sasa, anahitaji kuona maendeleo ya kikosi chake kabla ya kurejea
nyumbani kwa mchezo dhidi ya Mbweha wa Jangwani Algeria.
Stars iliyowasili jijini Johannesburg jumatatu mchana, imefikia
katika hoteli ya Holiday Inn Express iliopo katika eneo la Woodmead
ambapo imekua ikifanya mazoezi yake asubuhi na jioni katika viwanja vya
St. Peters College na kituo cha cha michezo cha Edenvale.
Kuhusu hali ya kambi, kocha mkuu wa Stars Charles Mkwasa amesema
anashukru maendeleo ni mazuri vijana wake wote wapo katika hali nzuri
hakuna majeruhi na wanaendelea na maaandalizi ya mchezo dhidi ya Algeria
utakaopigwa Novemba 14 jijini Dar es salaam.
"Dhumuni la
kuweka kambi huku ni kupata nafasi ya kuwaanda vijana kwa mazoezi katika
mazingira mazuri ikiwamo viwanja vya mazoezi, chakula na malazi
kinachopelekea kuongezeka kwa umakini katika mazoezi" Alisema Mkwasa.
"Tumeanza na mazoezi ya kujenga utimamu wa mwili kwa wachezaji, nguvu
na stamina, pumzi ili kuhakikisha vijana wote wanakua katika kiwango
sawa (fitness level) kisha tutaendelea na mazoezi ya kiufundi kwa siku
zilizosalia kabla ya kurejea nyumbani" aliongeza Mkwasa.
Wachezaji 26 waliopo kambini ni magolikipa Ally Mustafa, Aishi Manula
na Said Mohamed, walinzi ni Shomari Kapombe, Juma Abdul, Ramadhan
Kessy, Mohamed Hussein, Mwinyi Haji, Hassan Isihaka, Salim Mbonde,
Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub “Cannavaro”.
Wengine ni Himid Mao, Frank Domayo, Mudahir Yayha, Salum Abubakar,
Said Ndemla, Jonas Mkude, Salum Telela, Farid Musa, Saimon Msuva, Malimi
Busungu, Elias Maguri, John Bocco na Mrisho Ngasa.
Aidha wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea klabu
ya TP Mazembe ya Congo DR, wanatarajiwa kuungana na kikosi cha Stars
baada ya mchezo wao wa fainali Ligi ya Mabingwa Afrika Jumapili dhidi ya
USM Algiers.
0 comments:
Post a Comment