Wapenzi wa muziki nchini
ambao wanafuatilia onyesho la Coke Studio kupitia luninga ya Clouds ambalo
limeanza kuonyeshwa hivi karibuni wamesema linaleta burudani na Kolabo(mash-up)
za mwaka huu imeshirikisha wanamuziki wenye mvuto na kipaji kikubwa.
Wakitoa maoni yao baada ya
show ya nguli wa Bongleva Fid Q kutoka nchini na Maurice Kirya kutoka nchini
Uganda walisema onyesho hili mwaka huu limezidi kuwa bora na kuleta raha kwa
wapenzi wa muziki.
Walisema kuwa show hizi
zimerekodiwa kwa viwango vya juu vinavyokubalika kimataifa mbali na kushirikisha wanamuziki
wazuri wenye mvuto mkubwa katika anga ya muziki.
Jane Saimon Mwanafunzi wa
Chuo cha IFM kilichopo Dar es salaam anasema “Napenda sana Mash up ya Coke Studio iko bomba na imeshirikisha
wanamuziki wazuri.
Mkazi wa Mwanza
Aliyejitambulisha kwa jina la Dj.Pancras alisema kolabo (Mash up) za coke
Studio mwaka huu zinavutia kiasi kwamba yeye na wenzake siku ya onyesho hilo hawabanduki kwenye luninga.
Ally Katola wa Arusha
alisema “Coke Studio ni bomba kiasi
kwamba mimi na wenzangu hatukosi kamwe omnyesho hili ambalo lina wanamuziki
nguli kutoka nchini na nchi nyingine za Afrika”.
Suzana Mwakyoma wa Mbeya
anasema “Nampenda Vanessa na Ali Kiba na
kuwa kwao kwenye Coke studio kunalifanya onyesho hili liwe na mvuto mkubwa”.
Mustafa Abdul mkazi wa Tanga
anasema Coke Studio ni kisima cha burudani na ni onyesho mojawapo la muziki
lenye mvuto wa pekee kupitia kwenye luninga.
John Peter mkazi wa Moshi
anasema “Nimekuwa mpenzi wa onyesho la Coke studio tangia lilipoanzishwa na linaleta burudani kwa wapenzi wa muziki vijana kwa wazee.
Wasanii wanne kutoka Tanzania
waliopo kwenye show ya Coke Studio mwaka huu
ni Ben Pol ambaye anafanya mash up pamoja na mwanamuziki nguli kutoka Kenya anayejulikana
kama Wangechi, Fid Q anafanya mash up na Maurice Kirya kutoka Uganda, Gwiji wa
Bongo fleva nchini Ali Kiba anafanya mash up na Victoria Kimani kutoka
nchini Kenya na wakati Vanessa Mdee anafanya mash up na mwanamuziki nguli kutoka nchini Nigeria
ajulikanaye kama 2Face.
0 comments:
Post a Comment