Wafanyakazi wa kampuni ya Mobisol
wakikabidhi vifaa vya kuzalisha umeme wa jua kwa uongozi wa zahanati ya kijiji
cha Ngasamo wilayani Simiyu katika hafla iliyofanyika kijijini hapo
kuadhimisha kufikisha wateja 30,000 wanaonufaika na umeme wa kampuni hiyo.
*******************
*Mobisol yasherehekea mafanikio hayo kwa
kutoa msaada wa nishati katika zahanati ya kijiji cha Ngasamo wilayani Simiyu
Kampuni ya Mobisol yenye makao yake makuu mjini Berlini nchini ujerumani ambayo inajihusisha na uzalishaji wa umeme wa jua tayari imewaunganisha wateja wapatao 30,000 nchini Tanzania katika kipindi cha miaka 2 tangia ianze kutoa huduma hizi barani Afrika.
Kasi hii ya ongezeko la wateja wanaotumia umeme nishati ya jua
kutoka kampuni hii inadhihirisha kuwa uwekezaji wake unaendana sambamba na
kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania za kupunguza tatizo la upatikanaji
nishati ya umeme nchini.
Katika kuadhimisha mafanikio ya kufikisha idadi ya wateja 30,000
Mobisol imetoa msaada wa kuinganisha na umeme wa nishati ya jua zahanati ya
serikali ya kijiji cha Ngasamo kilichopo Simiyu ambapo anatokea mteja
aliyejiunganisha na umeme wa kampuni hiyo akiwa anakamilisha idadi ya wateja
30,000 katika nchi hizi mbili za Tanzania na Rwanda ambako inatoa huduma zake.
Akiongea wakati wahafla ya kutoa msaada huo iliyofanyika katika
zahanati hiyo,Meneja Masoko wa Mobisol,
bwana Nkora Nkoranigwa amesema kuwa kampuni hiyo imejizatiti kuondoa tatizo la
giza nchini na kuaikisha iawapatia wananchi umeme wa nishati ya jua wa uhakika
kwa kutumia teknolojia ya kisasa na gharama nafuu.BOFYA HAPA KWA KUSOMA ZAIDI.
“Sote tunaelewa kuwa nishati ya umeme inahitajika katika kuleta
maendeleo ya haraka na kuwaongezea vipato hususani wakazi wa
vijijini.Tutahakikikisa tunaunga mkono jitihada za serikali za kuzalisha na
kusambaza umeme kwa kwa wananchi hususani wanaoisi maeneo ya vijijini kwa
gharama nafuu ii uwasaidia katika itihada zao za kujiendelea kimaisha”.Alisema
Bwana Nkoranigwa Alisema umeme
ikipatikana utasaidia wananchi kuachana na matumizi ya vibatari na
kufurahia matumizi ya vifaa vya kisasa kama jokofu,feni ,kuchaji simu na
viginevyo na kuwezesha watoto kujisomea katika mazingira mazuri wawapo
majumbani na mashuleni hali ambayo
itasaidia kuongeza kiwango cha ufaulu katika masomo yao.
Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Bwana Patrick Onyango alishukuru kwa
msaada huo na kusema kuwa utawaondolea kero ya kukosa nishati ya umeme
waliokuwa nayo kwa muda mrefu na itarahisisha utoaji wa huduma za matibabu kwa
wagonjwa na aliahidi kuwa watahakikisha wanatunza vizuri vifaa vya nishati hiyo
walivyozawadiwa “Kuna msemo kuwa akufaaye kwa dhiki ndio rafiki wa
kweli”.Tunaishukuru kampuni ya Mobisol kwa msaada huu wa kusaidia wananchi
wengi”Alisema.
Naye Afisa Utawala wa Wilaya hiyo Bwana Rabani Mageja kwa niaba ya
serikali alishukuru kwa zahanati hiyo
kupatiwa msaada wa nishati na aliongeza kuwa serikali wilayani humo itazidi
kuunga mkono wawekezaji wanaokuja na miradi ya kusaidia kuleta maendeleo
katika jamii kama ulivyo mradi wa
nishati wa Mobisol.
Kwa upande wake mteja wa 30,000 wa kampuni ya Mobisol ambaye alisababisha
hafla hiyo kufanyika kijijini hapo na zahanati kupatiwa msaada Bwana Kichoro alisema
kuwa amefurahi kuona kampuni imemuenzi kwa kuleta msaada wa nishati kwenye
zahanati wa kuwanufaisha wananchi wote.
Akiwa ni mteja wa umeme unaozalishwa na kampuni hiyo alisema ni wa
uhakika na gharama nafuu na unafanya
maisha kuwa rahisi na kisasa na kuwataka wanakijiji wajiunge kwa aili ya kuishi
maisha ya kisasa na kuweza kuanzisha miradi midogo midogo ya uzalishaji kwa utumia
nishati hiyo.
0 comments:
Post a Comment