Nafasi Ya Matangazo

September 10, 2015

ALIYEKUWA Kaimu Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zuberi amechaguliwa kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania kuanzia leo. 

Sheik Zuberi amewashinda wagombea wengine watatu waliokuwa wakiwania nafasi hiyo ya juu ya kuwaongoza waislamu katika Mkutano mkuu wa Bakwata ulioshirikisha wajumbe zaidi ya 550 ambapo wajumbe 310 wa Baraza Kuu la Waislamu nchini (Bakwata) walipiga kura na kumchagua.

Mashekh wengine waliokuwa wakiwania nafasi hiyo ni pamoja na Ally Muhidin Mkoyogole, Khamis Abbas Mtupa na Hassan Ibrahim Kiburwa.

Mufti Zuberi anakuwa ni Mufti wa tatu kuchaguliwa kushika wadhifa huo akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Marehemu Muftu Issa Shaaban Bin Simba aliyefariki Juni 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mufti wa kwanza alikuwa Mufti Hemed Bin Jumaa bin Hemed. 

Kabla ya kuchaguliwa , Sheikh Abubakar Zuberi alikuwa Naibu Mufiti wa Sheikh Mkuu wa Tanzania na pia Mjumbe wa Baraza Kuu la Ulamaa nchini. 
Posted by MROKI On Thursday, September 10, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo