Rais Kikwete akimpa pole mmoja wa majeruhi Bw. Kokoliko Ramadhani akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo.
Watu wawili walipoteza maisha, akiwemo mvulana wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Abdallah na mwanamama Grace George (42), baada ya kumia katika msongamano mkubwa uliotokea katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni wa CCM katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015.ambapo jumla ya watu 17 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini hapo. Hadi jioni ya jana majeruhi saba walikuwa wameruhusiwa
Watu wawili walipoteza maisha, akiwemo mvulana wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Abdallah na mwanamama Grace George (42), baada ya kumia katika msongamano mkubwa uliotokea katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni wa CCM katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015.ambapo jumla ya watu 17 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini hapo. Hadi jioni ya jana majeruhi saba walikuwa wameruhusiwa
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimpa pole mmoja wa majeruhi Bi Flora Maduka akiwa kitandani pake hospitalini hapo baad ya kujeruhiwa katika msongamano huo
Rais Kikwete akimpa pole mmoja wa majeruhi Bi. Jalia Mohamed akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo
Rais Kikwete akiendelea kutoa pole kwa majeruhi
"Pole sana...." Rais Kikwete akimfariji mmoja wa majeruhi
Rais Kikwete alitumia wasaa huo kuwapa pole wagonjwa wengine waliokuwa wamelazwa wodi moja na majeruhi hao. Hapa anamfariji mtoto aliyeungua kwa moto
Rais Kikwete alitumia wasaa huo kuwapa pole wagonjwa wengine waliokuwa wamelazwa wodi moja na majeruhi hao. Hapa anamfariji mtoto aliyevunjika mguu wakati akicheza kwenye mti
Rais Kikwete akimpa pole mvulana ambaye aligongwa na gari wakati akielekea kumsikiliza mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana
Rais Kikwete alipata fursa ya kutembelea wodi ya watoto na kuwapa pole kwa kuumwa kwao
Rais Kikwete akiongea na wanafunzi waliokuwepo hospitalini hapo kumtembelea mgonjwa
Rais Kikwete alizongwa na wananchi waliokuwa na hamu ya kuongea naye
Rais Kikwete akitoa mapendekezo ya kupanua hospitali hiyo ambayo ina eneo kubwa lakini majengo machache ya chini. Alipendekeza uongozi wa hospitali na mkoa ubuni namna ya kuipanua kwa kujenga majengo ya ghorofa ili kuwepo na wodi na sehemu nyingi zaidi za huduma.
Mwishoni Rais Kikwete aliongea na wanahabari wa kutoka vyombo mbalimbali na kueleza masikitiko yake kwa yaliyotokea jana Uwanja wa Jamhuri baada ya mkutano wa kampeni kumalizika.
Rais Jakaya Kikwete akiongea na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya baada ya kuwajulia hali majeruhi wa msongamano baada ya mkutano wa kampeni uwanja wa Jamhuri Morogoro jana. PICHA NA IKULU
0 comments:
Post a Comment