Wahitimu wa darasa la saba kutoka shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini
Dar es salaam wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi Mhandisi Michael Mrema kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (hayupo pichani) wakati
wa mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika hivi karibuni shuleni
hapo.
Mgeni Rasmi
Mhandisi Michael Mrema akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi wa
shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam iliyofanyika hivi
karibuni shuleni hapo. Waliopo meza kuu ni Wakurugenzi wa shule hiyo, kwanza
kulia ni Mkurugenzi Imelda Philip akifuatiwa na Machage Kisyeri. Na wa kwanza
kushoto ni Julius Rutabanja.
Mtimu wa darasa la
saba wa shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam Deniol
Msemwa akipokea cheti cha kuhitimu elimu ya shule ya msingi kutoka kwa Mgeni
Rasmi Mhandisi Michael Mrema kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi
Evarist Ndikilo.
Mgeni Rasmi
Mhandisi Michael Mrema (katikati mstari wa mbele walioketi) akiwa katika picha
ya pamoja na Wahitimu wa darasa la saba kutoka shule ya Msingi Genius King’s
iliyopo jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa wakionesha vyeti
mara baada ya kukabidhiwa vyeti hivyo wakati wa mahafali ya nne ya kuwaaga
wanafunzi hao iliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo.
Mhitimu wa darasa
la saba Emma Emily akiwa amepokea cheti cha kufanya vizuri katika somo la
Hisabati pamoja na hati ya ufadhili wa kusomeshwa kidato cha kwanza hadi cha
nne katika shule ya sekondari ya Bright Future Girls iliyopo jijini Dar es
salaam.
Baadhi ya wazazi na
walezi wakifuatilia hafla ya kuwaaga Wahitimu wa darasa la saba kutoka shule ya
Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment