Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akimkabidhi kijana Iddy Abdallah Chilumba, msaada wa vifaa mbalimbali vya kubangulia korosho na pikipiki mpya, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla iliyofanyika kwenye sehemu yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Relwe, Manispaa ya Mtwara jana. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew Masatu (wa pili kushoto), Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Happy John (wa tatu kushoto) na Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.
***************
KAMPUNI ya simu za mkononi ya
Airtel imemuwezesha mjasiriamali Idd Chillumba vifaa vya kufanikisha shughuli zake za kufungasha Korosho ikiwa ni pamoja na usafiri wa kuwezesha kusambaza bidhaa zake kwa wateja wake kupitia mpango wake wa Airtel Fursa ambapo vitamuwezesha kuinua maisha yake na familia yake.
Akikabidhi vifaa hivyo meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi amesema, vifaa hivyo vitamuwezesha Bw. Chillumba kuendeleza biashara yake ya kufungasha Korosho na kusambaza kwa uharaka zaidi kwa wateja wake.
Bi Bayumi amesema, mpango huo wa kuwawezesha wajasiriamali vifaa ni sehemu ya mpango wa kampuni hiyo wa kuwawezesha vijana wenye malengo mazuri na maisha yao, tabia nzuri, na wenye dhamira ya kujikomboa kimaisha na kuwa wafanyabiashara wakubwa hapo baadae.
“Sisi kama kampuni ya mawasiliano tumeona ni vizuri kushirikiana na vijana ili kuhakikisha tunawawezesha na kukuza mitaji yao ya biashara na kuweza kujiinua kiuchumi, kuweza kufikia ndoto zao na vile vile kuongeza ajira kwa vijana hapa nchini” alisema meneja huyo.
“Vifaa hivi vitamuwezesha bw. Chillumba kuongeza biashara yake na kupanua wigo wa kutoa huduma kwa wateja wake na usafiri huu wa pikipiki utampa nafuu ya kusafirishia bidhaa zake kutoka sehemu moja kwenda nyingine.” aliongeza Bi Bayumi Akipokea msaada huo Bw. Chillumba ameshukuru kwa vifaa na usafiri huo na kuahidi kuendeleza zaidi biashara hiyo ili kutimiza ndoto zake za kuwa mfanyabiashara mkubwa.
“Sikuamini kama siku moja ningeweza kufikia malengo yangu katika biashra hii. Mimi ni mtoto wa kwanza katika familia yetu. Nilizaliwa miaka ishirini na nne iliyopita. Baba yangu alifariki nikiwa na umri wa mwaka mmoja. Mama yangu hakuwa na uwezo wa kunifikisha mbali kielimu hivyo niliishia kidato cha nne.
Ilinilazimu kuanza maisha mapema
kwa kuanzisha biashara ya kubangua korosho, fedha ninayopatajapokuwa ni
kidogo naitumia kujikimu mimi mwenyewe, kumsaidia mamayangu na ndugu zangu.
Kutokana na msaada huu kutoka Airtel, naahidi kuongeza juhudi na kutumia vyema
msaada huu ili kuhakikisha nakuza na kuendeleza biashara yangu na kuinua vijana
wenzangu hapo baadae” alisema Chillumba.
Kampuni ya simu ya Airtel
inazunguka nchi nzima kukutana na vijana kwa lengo la kuwapa elimu ya ujasiriamali na asha kutoa uwezeshaji kwa vijana ili waweze kukuza mitaji yao.
0 comments:
Post a Comment