Nafasi Ya Matangazo

August 04, 2015


 Afisa kilimo daraja la kwanza  wa halmashauri ya mbulu  Peter Sangawe   akiwa anaomuonyesha  Mkuu wa mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera  jinsi ya kuifadhi  nafaka bila kutumia kemikali  
Mkuu wa mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera akiwa anakagua vitunguu vinavyolimwa na halimashauri ya mbulu
Mkurugeniz wa kampuni ya SaBSAI pangani  Enterprises Mr Feroz Kassam   akiwa anawaonyesha  wananchi waliotembelea  katika shamba darasa lao kuangalia Bontera  mbolea au dawa ambayo inatumika kuoteshea mazao ili kuwweza kurutubisha aridhi   ili mkulima aweze kunufaika,Aidha alisema kuwa mbolea hii au dawa hiii inaweza kumpunguzia mkulima garama mbalimbali  huku akitolea mfano kuwa mbolea hii inasaidia kufukuza wadudu ambao wanaweza kushambumazao yakiwa shambani

wananchi wakiwa wanashangaa tangawizi ambayo inalimwa  na halmashauri ya Same

Na Woinde Shizza,Arusha
Wakulima pamaja na wafugaji wametakiwa kufuata ushauri wa wataalamu  pamoja na kufanyia kazi mafunzo wanayopata  kutoka kwa wataalam  ili waweze kulima kilimo chenye tija

Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera wakati akitembelea baadhi ya mabanda yaliyokuwepo katika maonyesho ya nane nane  yanayoendelea katika viwanja vya Taso njiro jijini Arusha.
Alisema  kuwa  kumekuwa na tatizo la wakulima wengi kutofanyia kazi elimu wanaopewa  kwani wakulima wengi ambao wanapewa elimu wamekuwa wakichukuwa elimu izo na kuzikalia badala ya kuzifanyia kazi.

Alibainisha kuwa alitegemea wakulima  wa kubwa ambao wanapata mafunzo haswa katika kipindi cha msimu wa maonyesho ya kilimo  nane nane wangeweza kuchukuwa elimu hiyo na kuenda kuwafundisha wakulima wadogo ambao walishindwa kufika katika maonyesho hayo na kupata elimu badala yake wakulima hao wamekuwa wakipata mafunzo na kuyaweka bila kuwagawia wenzio.


Aidha alisema kuwa pamoja kuwa kunachangamoto kubwa ya hali ya hewa katika kipindi hichi lakini iwapo wananchi wangekuwa wanafaaata elimu ya wataalam wanayopewa wangekuwa wananufaika kwani wangewezakufanya kitu kulingana na hali ya hewa inavyokwenda akitolea mfano iwapo kama mkulima kabla ya kupanda mbegu angekuwa anaenda kutafuta ushauri kwa mtaalam basi kama ni maindi anaotesha basi angeshauriwa ni mbegu gani ingeweza kumfaa kwakipindi hicho.
“nchi hii tuna rasilimali nyingi kwakweli tukiangalia maziwa ,mito na mabonde kama kweli wananchi wetu hususa ni hawa wakulima wangekuwa wanafanyia kazi mafunzo ambayo wanapewa naimaini tungekuwa mbali kiuchumi kwa kupitia kilimo na ufugaji pia ajira zingepatikana na sio hivyo tu lakini ata tatizo la njaa kwa ajapa nchini kwetu lingekuwa ni historia tu lisingetukuta”alisema Bendera.
Aidha alitoa kwa kulima kuchagua viongozi wanao faa kama vile kauli mbiu ya sasa inavyosema Matokeo makubwa sasa tuchague viongozi  bora kwa maendeleo ya  kilimo na ufugaji
Posted by MROKI On Tuesday, August 04, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo