Naodha wa timu ya Moro Kids Dissy Job akinyanyua kombe la ubingwa la
Airtel Rising Stars baada ya kutawazwa mabingwa wa mkoa wa Morogoro.
Timu ya Moro Kids waki pozi na kombe la ubingwa baada ya kutawazwa
mabingwa wa mkoa wa Morogoro katika mashindano ya Airtel Rising Stars.
****************
Timu ya Moro Kids imeukwaa uchampioni wa mashindano ya soka ya vijana
chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Morogoro
baada ya kuwafunga Kihonda 2-1 katika mchezo wa funga dimba uliopigwa
jana kwenye uwanja wa Shujaa mjini Morogoro.
Ushindi huo kwenye mchezo wa jana uliohudhuriwa na mashabiki wengi
uliwawezesha Moro Kids kufikisha pointi sita wakifuatiwa na timu ya
Tecfort iliyohitimisha mashindano hayo ya mkoa ikiwa na pointi tatu.
Wakati huo huo chama cha soka mkoani Morogoro (MOREFA) kimetangaza
kikosi cha wachezaji 20 kitakacho uwakilisha mkoa huo katika
mashindano ya taifa yaliyopangwa kuanza kutimua vumbia kwenye uwanja
wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia Septamba 11 hadi
21.
Katibu Mkuu wa MOREFA Emmanuel Kimbawala amesema kikosi hicho
kilichochaguliuwa wakati wa michuano hiyo mkoani Morogoro kimeundwa na
wachezaji wenye vipaji na ku0nyedha dhamira ya dhati ya kuweza kutwaa
tena ubingwa wa Airtel Rising Stars ngazi ya taifa mwaka huu.
Lengo la mashindano ya Airtel Rising Stars ni kuwapa fursa wachezaji
chipukizi wa soka, wasichana na wavulana, kuonyesha vipaji vyao na
hatimaye kuweza kuonekana na kuchaguliwa kuchezea timu mbalimbali.
matunda ya Airtel Rising Stars yanaonekana katika timu za taifa za
vijana na Twiga Stars.
Mwaka huu mashindano ya Airtel Rising Stars yanajumuisha mikoa ya
kisoka ya Ilala, Temeke, Ilala Mbeya na Mwanza kwa timu za wasichana
na wavulana huku mkoa wa Morogoro ukishirikisha wavulana peke yake
wakati Arusha ni wasichana tu.
0 comments:
Post a Comment