Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini Tanzania(ERB) Muhandisi Steven Mlope
akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuelezea
mafanikio ya Bodi hiyo katika kipindi cha miaka 10 hasa ukuzaji wa sekta
ya ajira nchini Tanzania.
***********
Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini Tanzania (ERD) imefanikiwa
kutengeneza ajira 1600 kwa Watanzania kufuatia usajili wa makampuni 160
ya ushauri wa kihandisi yaliyoanzishwa nchini kote nchini katika kipindi
cha miaka 10 kuanzia mwaka 2005 hadi 2015.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuelezea mafanikio ya
Bodi hiyo kwa kipindi cha miaka 10 Msajili wa Wahandisi nchini Tanzania
(ERB) Muhandisi Steven Mlope amesema kuwa kwa kusajili makampuni 160
katika kipindi cha miaka 10 pia wamefanikiwa kusajili wahandisi wapatao
8496 ambao kwa ujumla wao wametengeneza ajira kwa Watanzania 256,480.
Amesema
katika kipindi cha miaka 10 Bodi hiyo imefanikiwa kuongeza kwa kiasi
kikubwa idadi ya wahandisi waliosajiliwa kutoka 6868 waliokuwepo nchini
Tanzania hadi 15,364 mwaka 2015.
Aidha
Muhandisi Mlope amesema kuwa Fani ya Uhandisi nchini Imeendelea kukukua
kutokana na uwepo wa wahandisi wa Majengo,wahandisi wa mazingira, Mifumo
ya kompyuta na wahandisi wa mazingira wanaofanya kazi zao kwa
kushirikiana.
Aidha, amesema kuwa Bodi ya
Usajili wa Wahandisi kwa kuzingatia sheria ya Bunge namba 15 ya mwaka
1997 iliyofanyiwa marekebisho, na sheria No.24 ya mwaka 2007 imepewa
majukumu ya kuratibu na kusimamia mienendo na shughuli za Kihandisi
zinazofanywa na wahandisi pamoja na makampuni ya ushauri wa kihandisi
nchini.
Ameongeza kuwa kwa mujibu Sheria ni
kosa kwa mtu binafsi,kikundi cha watu binafsi, kikundi cha watu au
kampuni yoyote kutoka ndani na nje ya nchi kufanya shughuli za kihandisi
bila kusajiliwa au kuwa na wahandisi wasiosajiliwa.
Ameeleza
kuwa katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2015 Bodi hiyo ilitoa onyo na
adhabu mbalimbali ikiwemo kufuta usajili wa wahandisi 330 waliokiuka
Sheria ya Bodi ya Usajili wa wahandisi.
Kwa
upande wa shughuli za kihandisi katika ngazi ya wilaya kote nchini
Muhandisi Mlope amesema kuwa kufikia mwaka 2015 hali imeendelea
kuimarika licha ya kuwepo kwa changamoto ndogondogo.
Muhandisi
Mlope amebainisha kuwa Bodi inaendelea kuratibu mpango wa Mafunzo
(SEAP) wenye lengo la kuwajengea uwezo wahandisi wanaohitimu masomo
katika vyuo mbalimbali ili waweze kukidhi viwango kuwawezesha vya
kuwawezesha kusajiliwa na Bodi hiyo.
"Mpango
huu wa mafunzo unaofadhiriwa na Serikali kwa lengo la kuwajengea uzoefu
wahitimu, kuwawezesha kuajiliwa na kupata uzoefu mapema umekuwa na
manufaa makubwa kwa nchi yetu"
Ametoa wito kwa
wenye viwanda na makampuni kuwapokea na kuwaajili wahandisi
waliosajiliwa na wale waliokula kiapo ili kazi wanazozifanya ziweze
kukidhi viwango vilivyowekwa.
Pia amesema kuwa
Bodi hiyo inaendelea kuwaendeleza wahandisi wataalaam waliopo nchini kwa
kuandaa mihadhara na kozi fupifupi ambazo huendeshwa na vyuo vinavyotoa
mafunzo ya kozi hiyo huku wao kama bodi wakitoa ithibati na kuandaa
makongamano ya wahandisi kila mwaka.
Amefafanua
kuwa Septemba 3 mwaka huu Wahandisi watakuwa na Kongamano kubwa la
mwaka litakalowakutanisha wahandisi wote nchini ili kuweza kukidhi
matarajio ya Wananchi kufuatia wengi wao kuongeza uelewa juu ya matumizi
ya wahandisi.
"Mwamko sasa umeongezeka
kutokana na Serikali kuendelea kuweka mkazo katika masomo ya Sayansi na
ujenzi wa maabara ili kuzalisha wataalam wa kutosha wenye viwango"
Amesema.
Kuhusu maslahi ya wahandisi nchini
amesema kuwa wao kama Bodi wanaishukuru Serikali kwa kuendelea
kuboreshaji maslahi yao na kusisitiza kuwa jambo hilo linaendana na
mabadiliko ya uchumi yaliyopo ili kuwawezesha wataalam hao kufanya kazi
zao kwa ufanisi na kuheshimiwa na jamii wanayoitumikia.
0 comments:
Post a Comment