Vijana skauti 4 pamoja na kiongozi
mmoja ni miongoni mwa washiriki wa Jamboree ya
maskauti ya dunia itakayofanyika Nchini Japan katika mji wa Yamaguchi –
Kihara hama kuanzia tarehe 28 Julai hadi
8 Agosti 2015.
Jamboree ya Skauti ya Dunia ni
mkusanyiko wa Skauti kutoka nchi zote
wanachama na kawaida hufanyika kila baada ya miaka minne kama iliv yo kwa
mashindano ya mpira ya kombe la dunia.
Mwanzilishi wa Chama cha Skauti duniani Hayati Lord Baden Powell
alianzisha mfumo wa Jamboree ya Skauti
ya dunia kwa madhumuni ya kuwakutanisha vijana skauti kubadilishana mawazo na
kujifunza mambo mbalimbali kutoka nchi tofauti tofauti.
Jamboree ya kwanza ya maskauti ya dunia ilifanyika London Uingereza mwaka
1920 na kuanzia mwaka huo imekuwa ikifanyika kila mwaka katika nchi tofauti
tofauti.
Shirikisho la Vyama vya Skauti Dunia (WSB) World Scouts Bureau, ndio
hupanga na kuchagua nchi itakayo andaa
Kambi hili la kimataifa katika kipindi kijacho.
Chama cha Skauti Tanzania inapeleka idadi ndogo ya washiriki kutokana na
gharama kubwa za ushiriki wa kambi hii. Jumla ya dola za kimarekani 4000 sawa
na milioni 8 za Kitanzania ndio gharama za ushiriki kwa mshiriki mmoja.
Gharama hizo ni pamoja na usafiri, chakula malazi na ada ya ushiriki wa
kambi hiyo ambayo huchukua karibu siku 10.
Shughuli zinazofanyika wakati wa Jamboree hiyo ni pamoja na mafunzo mbalimbali
ya stadi za kiskauti, kazi za Jamii, Moto wa Kambi, na siku moja maalum ya
Kimataifa ambapo kila nchi wanachama huandaa maonyesho maalum kuonyesha bidhaa
mbalimbali walizonazo ikiwa ni pamoja na kuonyesha utamaduni wao.
Kikosi cha skauti kutoka Tanzania kinawakilishwa na:-
Eline Kitali – Kamishna
Mtendaji na Mkuu wa Msafara.
Michael Malima kutoka mkoa
wa D’salaam
James Mzoma Chinula kutoka
mkoa wa Kilimanajaro
Malkia Ulimboka Mwakilili
kutoka mkoa wa Mbeya
Martha Albert Bennie.
Kutoka mkoa wa Mwanza.
Skauti hao wanatarajia
kuondoka nchini Jumamosi tarehe 25 Julai 2015 na shirika la ndege la Emirates muda wa saa 10.45 alasiri na wanatarajia kurejea nchini 10 Agosti 2015.
HIDAN .O. RICCO.
KAMISHNA MKUU MSAIDIZI
HABARI NA MAWASILIANO.
0 comments:
Post a Comment