MKURUGENZI Mkuu wa kwanza wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha Mshomba, akiwasilisha mada wakati wa warsha iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa Wahariri kwenye Hoteli ya Court Yard jijini Dar es Salaam, Julai 22, 2015
Na
K-VIS MEDIA
MFUKO
wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), umekutana na Wahariri wa vyombo vya Habari
Nchini, kwenye Hoteli ya Court Yard jijini Dar es Salaam, Julai 22, 2015, kwa
nia ya kujitambulisha na kuelezea mikakati yake ya kiutendaji na majukumu iliyo
nayo.
Akiwasilisha
mada kwa Wahariri hao, Mkurugenzi Mkuu wa Kwanza wa Mfuko huo, Masha Mshomba,
amesema, Mfuko huo umeanzishwa ili kutekeleza sheria ya fidia kwa wafanyakazi
(Sheria namba 20, ya mwaka 2008.
“Majukumu
ya Mfuko huu ni kuwasaidia wafanyakazi wanaoathirika kuweza kurudi kazini au
kushiriki katika shughuli nyingine zitakazowapa kipato.” Alisema Mshomba na
kuongeza kuwa majukumu mengine ni pamoja na kutunza kumbukumbu za matukio ya
ajali, magonjwa na vifo vinavyotokana na kazi, ikiwa ni pamoja na kuelimisha
umma kuhusu kazi za mfuko na manufaa yake.
Alisema,
Mfuko huo ni mpya na kwamba unahitaji ushirikiano wa dhati kutoka vyombo vya
habari na ndio maana Mfuko umeona umuhimu wa kukutana na Wahariri wa vyombo vya
habari kwani wao ndio kiungo kati ya Mfuko na Umma.
Akifungua
warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii, (SSRA), Irine Isaka, amesema, Mfuko huo umekuja kurahisisha ushughulikiwaji wa malalamiko ya fidia kwa wafanyakazi moja kwa moja bila ya kuanza kupitia sehemu
nyingine.
Alisema,
SSRA kama mama wa Mifuko yote, inao wajibu wa kuisaidia WCF katika kutekeleza
majukumu yake ya kisheria na Wahariri wa vyombo vya Habari ni kiungo muhimu
katika kuhakikisha umma wa Watanzania unajua shughuli na kazi za Mfuko huo.
Naye
kwa upande wake, Katibu wa Jukwaa la Wahariri, Neville Meena alishukuru WCF kwa
kuwaalika wahariri ili kuwaeleza vema shughuli na majukumu ya Mfuko huo kwani
vyombo vya habari ndio wakala wa Umma na taasisi za kutoa huduma kama WCF.
Ninawapongeza
WCF kwa kuwa majasiri wa kuwaalika wahariri na kukutana nao na kupokea maswali
yao, kwani taasisi nyingine huogopa kufanya hivyo tena katika hatua ya awali
kama yenu. Alisema Meena
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Irine Isaka, akifungua warsha hiyo
Mhariri Shemax Ngahamera akizungumza kwenye warsha hiyo
Mhariri wa vipindi wa ITV/Radio One, Steven Chuwa, (kulia), na Mhariri Mtendaji wa EFM, Scolastica Mazula, wakipitia mada zilizokuwa zikitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF
Mhariri Mshiriki wa gazeti la Nipashe, Ramadhan Mbwaduke, akiuliza swali
Mhariri gazeti la Serikali, Sunday News, Ichikaeli Maro, akizungumza wakati wa warsha hiyo
Baadhi ya Wahariri wakinukuu yaliyokuwa yakielezwa kwenye warsha hiyo
Mhariri Anold Victor, akiuliza swali
Mhariri mkongwe, Mzee Yasin Sadick, akifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye warsha hiyo
Baadhi ya Wahariri, wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa juu ya kazi na huduma zitolewazo na WCF
Mhariri wa kujitegemea Mzee Wence Mushi akiuliza swali
0 comments:
Post a Comment