MWANAMAMA aliyepata kuwa Mwenyekiti mwenza wa Bunge maalum la Katiba na Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rasi Muungano, Samia Hassan Suluhu ndie mgombea mwenza wa Dk John Pombe Magufuli katika mbio za kuwania Urais katika uchaguzi ujao.
Wawili hao watachuana na wagombea kutoka Kambi ya upinzani ambao huenda mwaka huu wakasimamisha mgombea mmoja.
Samia Hassan Suluhu alizaliwa Januari 27, 1960 na ni Mbunge wa Jimbo la
Makunduchi Zanzibar .
Pia Aliwahi
kuwa Waziri katika wizara za Utalii, Biashara na Uwekezaji, Waziri wa Kazi
Jinsia na Watoto katika serikali ya
Mapinduzi Zanzibar.
Mwaka 1966-1968, alisoma shule ya msingi Chwaka mjini
Unguja na mwaka 191970-1971 alisoma shule ya Msingi Ziwani, Pemba na kuhamia
Mahonda Shule ya Msingi mjini Unguja mwaka 1972.
Mwaka 1973-1975 alisoma Sekondari ya Ngambo mjini Unguja, na
mwaka 1976 Lumumba nayo ya Unguja.
Mwaka 1989 alisoma National Institute of Public
Administration, Lahore Pakistan, Institute of Management for Leaders, Hyderabad
India 1991 na Zanzibar Institute of
Financial Administration, ZIFA 1983.
Mwaka 1983-1986 alisoma Taasisi ya Uongozi
Mzumbe (IDM) sku hizi Chuo Kikuu Mzumbe.
Na kasha akaenda Chuo Kikuu cha Manchester,
London mwaka 1992 - 1994
Baade
mwaka 204-2005 alikua Chuo Kikuu Huria cha Southern New Hampshire, USA
0 comments:
Post a Comment