Katikati
ni Meneja Mahusiano shirika la The Foundation For Tommorow ,Anton
Asukile akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Arusha juu ya
Kampeni ya SHAMIRI inayolenga kuchangisha milioni 50 kwa ajili ya
kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi ,kulia ni Meneja
Programu wa masuala ya kijamii na afya Hedwiga Mchaki na kushoto ni
Hilda Lema Mfanyakazi wa shirika hilo(Habari Picha na Pamela Mollel wa
jamiiblog)
Meneja Programu wa masuala ya kijamii na afya wa shirika la The Foundation For Tommorow Hedwiga Mchakiakifafanua jambo katika kikao na waandishi wa habari jijini Arusha
Hilda Lema mfanyakazi wa shirika hilo anasisitiza jamii kushiriki katika kampeni hiyo
Taswira
Mwanafunzi
wa chuo kikuu Nicemary Phelix aliyewezeshwa na shirika la The
Foundation For Tommorow kwa kusomeshwa kwanzia darasa la nne hadi sasa
yupo elimu ya juu baada ya kupoteza wazazi wake wote, anaomba watanzania
kuonyesha hisia zao katika kusaidia jamii yenye uhitaji na siyo
kusubiria wafadhali kutoka nje ya Nchi Shirika lisilo la kiserikali la The Foundation for Tommorow limezindua kampeni ya kuchangia SHAMIRI ya kusaidia elimu ya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu lengo ni kuchangisha kiasi cha shilingi milioni 50 zitakazowawezesha kupata elimu bora na kuondokana na mazingira yanayowakabili.
*************
Meneja Mahusiano wa shirika hilo Anton Asukile alisema hayo jana akizindua kampeni maalumu ya SHAMIRI inalenga kusaidia ustawi wa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
“Kampeni hii itawezesha kuinua uchumi wa kaya 40 za watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi kupitia mradi wa WEZESHA KAYA pia itasaidia upatikanaji wa vifaa muhimu vya kujifunzia kwa watoto wapatao 112” Alisema AntonAsukile ameiomba jamii ya Watanzania kushiriki katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili jamii ili kuwakomboa watoto wanoishi katika mazingira hatarishi kwa kuchangia kampeni ya SHAMIRI.
Alisema kuwa Watanzania wataweza kuchangia fedha hizo kwa njia ya simu katika kampeni hiyo imeanza rasmi mwenzi Julai na itahitimishwa septemba 25 mwaka huu.
Meneja Programu wa masuala ya kijamii na afya Hedwiga Mchaki amesema kuwa baada ya kutoa misaada kwenye familia duni wameona ni vyema wakazipatia mafunzo ya ujasiriamali na mikopo ili waweze kujikwamua na kusomesha watoto wao pasipo kutegemea misaada.
Hedwiga ameitaka jamii ya watanzania kuamka na kusaidia watoto yatima na wanaotoka kwenye familia masikini badala ya kusubiri mashirika kutoka nje yaje kutoa misaada.
0 comments:
Post a Comment