Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu,Damian Lubuva (katikati) akizungumza na waandishi habari juu
juu ya maendeleo mbalimbali katika kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika leo Makao
Makuu ya NEC jijini Dar es Salaam,Kulia Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar
es Salaam,Kamishina Suleiman Kova na Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji
Uchaguzi,Clothilde Komba.
Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu
ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akizungumza na waandishi habari juu
juu jeshi la polisi lilivyojipanga
katika suala la ulinzi kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika leo Makao Makuu ya
NEC jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa
Globu ya Jamii)
************
Na
Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
TUME
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kuanza kutoa fomu ya urais ,Ubunge pamoja
na Udiwani kesho na kumalizika kwa zoezi la utoaji fomu hizo ni Agasti 21 mwaka
huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi,Jaji Mstaafu,Damian Lubuva amesema wakati wa uchukuaji wa fomu
ya urais itatolewa bure lakini wakati wa kurudisha anatakiwa kuweka dhamana ya
Sh.milioni Moja na wadhamini wadhamini 200 katika kila mkoa na kuwepo kwa mikoa
miwili Zanzibar.
Lubuva
a amesema kuwa wakati wa kuchukua fomu viongozi wa vyama vya kisiasa wanatakiwa
kuchukua fomu na kurudisha bila kuwa na kundi kubwa ambalo linaweza kusimamisha
shughuli za watu wengine.
Amesema
kwa fomu za ubunge ni sh.50,000 na udiwani sh.5000 ambapo wanatakiwa
kuchukulia katika ofisi za wilaya na uchukuaji huo lazima uwe wa kistaarabu
katika kuweza watu wengine waendelee na shughuli zao.
Lubuva
amesema kuwa wanasiasa wanatakiwa na lugha za kistaarabu katika
mikutano yao katika kujenga demokrasia iliyo ya ukweli.
Hata
hivyo amesema kuna baadhi ya vijana wanauza kadi za tume ya taifa ya uchaguzi
na kutaka vyombo vya usalama kuchunguza pamoja na kuwachukulia hatua watu
wanaouza kadi hizo.
Kamanda
wa Polis wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova amesema kuwa
uchaguzi unaendana na usalama hivyo jeshi limejipanga katika ulinzi
katika kipindi hiki.
Kova
amesema kuwa Jeshi litaendelea kushirikiana na viongozi wa siasa katika kuleta
amani katika kipindi cha uchaguzi.
0 comments:
Post a Comment