Afisa Habari wa Coastal Union, Assenga Oscar
KUFUATIA vikao vya maridhiano ya
Uhakiki wa wanachama wa Klabu ya Coastal Union ulioongozwa na Mjumbe wa Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la soka nchini (TFF) Ahmed Iddi Mgoyi.
Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa
Selestine ameiandikia barua Klabu ya Coastal Union akiiagiza klabu hiyo
kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa wanachama tarehe 17 Mei mwaka 2015.
Matokeo ya maamuzi haya yamepatikana
baada ya kikao cha usuluhishi cha amani kilichoongozwa na Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya TFF, Ahmed Iddi Mgoi aliyekuwa ameongozana na Makamu Mkurugenzi wa
Sheria na Uanachama shirikisho la soka nchini (TFF) Eliud Peter Mvella
kilichofanyika April 13 mwaka huu katika hotel ya Tanga Beach Resort Tanga
mjini.
TFF imehaidi kutuma orodha tatu za
majina
(A) Wanachama stahiki.
(B) Wanachama waliobainika kuwa wanadosari na inabidi wathibitishwe na
wanachama stahiki na.
(C) Waombaji wapya wa wanachama watakaohakikiwa
na wanachama stahiki.
Orodha hizi zinapaswa kubandikwa
kwenye ubao wa Matangazo wa Klabu, katika kikao cha ufunguzi cha kuleta
usuluhisho huo, mbali na kuhudhuriwa na kamati ya Utendaji ya Coastal Union
chini ya Makamu wake Mwenyekiti Steven Mguto pia kilihudhuria na Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya TFF,Khalid Abdallah, Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa wa
Tanga,Said Soud.
Wengine waliohudhuria kikao hicho
walikuwa ni Afisa Michezo wa Mkoa wa Tanga, Digna Tesha, Katibu wa Chama cha
soka Mkoa wa Tanga, Beatrice Mgaya, Afisa Utamaduni Jiji la Tanga, Peter
Semfuko na Katibu wa Chama cha soka wilaya ya Tanga (TDFA) Salim Carlos.
0 comments:
Post a Comment