BB King akiangalia maashabiki wake baada ya kutumbuiza katika moja ya maonesho yake.
Rais wa Marekani Barack Obama akimba moja ya nyimbo za BB King katika moja ya tajasha lake alilohudhuria huko Marekani.
BB King enzi za uhai wake akiwa kazini.
MKALI wa muziki wa bluzi duniani Riley B
King au maarufu kwa jina la B.B. King amefariki
dunia.
Taarifa zilizotolewa na Mwanasheria wake, Brent
Bryson kwa shirika la Habari la AP, zilisema kuwa King alifariki akiwa
usingizi majira ya saa 9:40 usiku wa
kuamkia leo nyumbani kwake Las Vegas.
B.B King alizaliwa Septemba 16, 1925 huko Itta Bena, Mississippi, nchini Marekani,
amekuwa muimbaji wa muziki huo wa bluzi, mtunzi na mpiga gitaa maarufu duniani
amefariki akiwa na umri wa miaka 89.
King atakumbukwa na wengi hasa wapenzi wa muziki
wa bluzi jinsi alivyoweza kuteka na kukionga nyoyo za wapenzi wengi wa muzki na
kuwavutia vijana kuupenda mziki huo hasa kwa wimbo wake wa “The Thrill Is
Gone.”
King ameuza nyimbo zake zaidi ya mamilioni
duniani kote na pia ni mmoja wa wasanii walioko katika Blues Foundation Hall of
Fame na ile ya Rock and Roll Hall of Fame.
Mwaka 2009 alishimnda
tuzo maarufu duniani za 15 za Grammy katika kundi la Bluzi asilia aliyoishinda
kupitia albam yake ya “One Kind Favor.”
0 comments:
Post a Comment