Wanawake
wa TFDA walikuwa ni sehemu ya waliojitokeza katika kushiriki na
kufanikisha Maadhimisho hayo
yaliyofanyika katika ngazi ya mkoa (Dar Es Salaam) ambapo Mgeni Rasmi alikuwa
ni Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete.
Kauli
mbiu ya inasema “UWEZESHAJI WANAWAKE;
TEKELEZA WAKATI NI SASA” ambayo inalenga kuhamasisha jamii kutambua mchango
wa Wanawake katika kuleta maendeleo yao; na kuelimisha wadau mbalimbali
kuangalia upya wajibu wao wa kuwashirikisha wanawake na kuwapa haki sawa katika
nafasi za elimu, uchumi na kijamii ili waweze kuwa chachu katika kuleta
maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Kwa
kutambua dhima hiyo, pamoja na mambo mengine, Wanawake wa TFDA walitoa elimu
inayopiga vita matumizi ya “mikorogo” kwa vile inachangia kuhatarisha afya ya
mwanamke na jamii. Ili kufikisha ujumbe huo walitumia mbinu mbalimbali kama
baadhi ya picha zinavyoonesha hapa chini:
Wanawake wa TFDA wakisubiri kushiriki maandamano ya aiku ya mwanamke Duniani jijini Dar es salaam jana.
Ilikuwa ni miserebuko ya akina mama na wadada.
Father Kidevu,
ReplyDeleteWaambie hao watu wa TFDA waendelee kwa sana kupiga vita mikorogo na vipodozi vilivyopigwa marufuku Tanzania, vitatumaliza
Big up TFDA........MKOROGO NOMAAA
ReplyDelete