Nafasi Ya Matangazo

March 12, 2015

 Mratibu wa Mradi wa Macho kwa shule za msingi kupitia mradi wa afya ya macho kwa mtoto unaofadhiliwa na benki ya Standard Chartered (Seeing is Believing)  kutoka shirika lisilo la kiserikali la Brien Holden Vision Institute Violeth Shirima  (kushoto) akimkabidhi msaada wa sanduku la vifaa vya macho  vyenye thamani ya shilingi milioni 48 Muuguzi Msaidizi wa Huduma za Macho wa Hospitali ya  Wilaya ya Kyela, Monica Francis (kulia) wakati wa hafla iliyofanyika katika hospitali ya mkoa wa Mbeya.  Wanafunzi wa shule za msingi za halmashauri za Mbozi, Ileje , Kyela watanufaika  na msaada huo  wa kutibiwa magonjwa ya macho bure. Wanaoshuhudia:  wa pili kutoka kulia ni Kaimu Afisa Elimu wa Wilaya ya Kyela,  Kassim Mtili na Mratibu wa Huduma za Macho Mashuleni,   Leah Mwakakapala.
 Kaimu  Katibu  Tawala Mkoa wa Mbeya, Constantine Mushi akikabidhiwa  msaada wa sanduku  la  vifaa vya macho na Mratibu wa Huduma za Macho kwa watoto wa shule za msingi  kupitia mradi wa Afya ya Macho  kwa Mtoto (Seeing is Believing) unaofadhiliwa na benki ya Standard Chartered, Violeth leth Mushi ,wakati wa hafla iliyofanyika katika hospitali ya mkoa wa Mbeya. Jumla ya vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 48 vilikabidhiwa kwa hospitali za wilaya za Mbozi, Ileje na Kyela. Mradi huo utawanaufaisha wanafunzi  wa wilaya hizo kwa kupata matibabu bure pamaoja na miwani mara baada ya kugundulika kama wanamatatizo ya macho ili weweze kusoma vizuri.
 Mratibu wa Taifa wa Huduma za Macho, Dkt.Nkundwe Mwakyusa (kushoto) akiwaelekeza  wataalamu wa macho kutoka katika hospitali ya Wilaya ya Kyela  jinsi  ya kutumia vipimo vya macho mara baada ya kukabidiwa msaada wa vifaa  hiyo vyenye thamani ya shilingi milioni 48. Kulia ni Muuguzi Msaidizi wa hospitali hiyo Monica Francis, Kaimu Afisa Elimu  Wilaya Kassim Mtili na Mratibu wa Huduma za Macho  Mashuleni wa Wilaya Leah Mwakapala, mradi huo umefadhiliwa na benki ya Standard Chartered  kwa wilaya za mkoa wa Mbeya na Mwanza. Wa pili kutoka kushoto ni Mratibu wa Macho Mashuleni  toka shirika lisilo la kiserikali la Brien Holden Vision Institute, Violeth Shirima.
 Mratibu wa Taifa wa Huduma za Macho, Dkt.Nkundwe Mwakyusa (katikati) akisistiza jambo wakati alipokuwa akiongea na wataalamu wa macho kutoka katika wilaya za Kyela ,Ileje,na Mbozi (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 48, vilivyotolewa na Shirika lisilo la kiserikali la Brien Holden Vision Institute  kupitia mradi wa Afya ya Macho Mashuleni (Seeing is Believing) unaofadhiliwa na benki ya Standard Chartered kwenye hospitali za wilaya hizo za mkoa wa Mbeya. Kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Constantine Mushi na Mratibu wa mradi huo Violeth Shirima.
 Mratibu wa Mradi wa  Huduma za Macho Shule za Msingi  unaofadhiliwa na benki ya Standard Chartered (Seeing is Believing)  kutoka shirika lisilo la kiserikali la Brien Holden Vision Instutite, Violeth Shirima  (kulia) akimkabidhi msaada wa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 48 Muuguzi Msaidizi wa Huduma za Macho wa Hospitali ya  Wilaya ya Kyela, Monica Francis (wa tatu toka kushoto) wakati wa hafla iliyofanyika katika hospitali ya mkoa wa Mbeya.  Wanafunzi wa shule za msingi za halmashauri za Mbozi, Ileje na Kyela watanufaika  na msaada huo  wa kutibiwa magonjwa ya macho bure.
Mratibu wa Mradi wa  Huduma za Macho Shule za Msingi  unaofadhiliwa na benki ya Standard Chareterd (Seeing is Believing)  kutoka shirika lisilo la kiserikali la Brien Holden Vision Institute, Violeth Shirima  (kulia) akimuonyesha Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya miwani inayotengenezwa na shirika lake  kwa ajili ya kuwagawia watoto mashuleni  wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wavifaa vya macho  vyenye thamani ya shilingi milioni 48 kwa hospitali za wilaya za Mbozi, Ileje na Kyela zote za Mkoani Mbeya.
Mratibu wa Mradi wa  Huduma za Macho Shule za Msingi unaofadhiliwa na benki ya Standard Chartered (Seeing is Believing)  kutoka shirika lisilo la kiserikali la Brien Holden Vision Institute, Violeth Shirima  (kulia) akimkabidhi  msaada wa sanduku la vifaa vya macho  vyenye thamani ya shilingi milioni 48 Muuguzi Msaidizi wa Huduma za Macho wa Hospitali ya  Wilaya ya Kyela, Monica Francis (kulia) wakati wa hafla iliyofanyika katika hospitali ya mkoa wa Mbeya ambapo wanafunzi wa shule za msingi za Halmashauri za Mbozi, Ileje na Kyela watanufaika  na msaada wa kupima macho na kutibiwa magonjwa ya macho bure.
Kaimu Afisa Elimu wa Wilaya ya Kyela Kassim Mtili (kulia), Mratibu wa Huduma za Afya Mashuleni wa wilaya hiyo,  Leah Mwakapala (katikati) na Muuguzi Msaidizi wa Huduma za Macho wa Hospitali ya  Wilaya ya Kyela, Monica Francis  wakikagua mashine ya komputa ya kupima macho mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vifaa vya macho  vyenye thamani ya shilingi milioni 48  na Mratibu wa Mradi wa  Huduma za Macho Shule za Msingi unaofadhiliwa na benki ya Standard Chareterd (Seeing is Believing)  kutoka shirika lisilo la kiserikali la Brien Holden Vision Institute Violeth Shirima (kulia) wakati wa hafla iliyofanyika katika hospitali ya mkoa wa Mbeya.
Posted by MROKI On Thursday, March 12, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo