Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute Eden Mahayo (Pwani.kushoto)akimkabidhi
msaada wa sanduku la vifaa vya kupimia macho Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Mkuranga Mbenjamin Majoya kwa
ajili ya wanafunzi wa shule za msingi 122 za
Mkuranga ambapo wanafunzi hao
watapata huduma ya kupima na kutibiwa macho bure.hafa hiyo ilifanyika hivi
wilayani 002mkuranga mkoa wa Pwani.
Matroni wa haospitali ya wiraya ya Mkuranga Mkuranga
Rosemary Magombola akisoma moja ya
maneno kwenye kibao maarumucha kupimia macho mara baada ya kukabidhiwa msaada
huona taasisi isiyo ya kiserikali ya Brien
Holden Vision Institute Eden kwa ajili
ya wanafunzi wa shuleza msingi 122
.Kulia ni Mratibu wa taifa wa huduma za macho Dkt.Nkundwa Mwakyusa (kushoto)
Mratibu wa mradi huo kwa watoto wa shule za msingi toka taasisis ya ya Brien Holden Vision Institute Eden ,Rebecca
Kasika.
Afisa maendeleo ya jamii ya mji wa kibaha mkoa wa
pwani akikabidhiwa na Mashine ya kupimia macho na Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali
ya Brien Holden Vision Institute Eden
Mahayo (kushoto) wakati wa hafla ya kukabidhi
wa msaada wa vifaa vya macho vyenye
thamani ya shilingi milioni 11.4 kwa
ajili ya kuwahudumia wanafunzi wa Wilaya
hiyo ya Kibaha ambao watanufaika na huduma
hiyo ya upimaji macho pamoja na matibabu bure
Wafanyakazi wa hospitali ya Kibaha kitengo cha macho
wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa ya
Brien Holden Vision Institute Eden,mara baada ya kukabidhiwa msaada wa
vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4.
***********
NA MWANDISHI WETU
TAASISI isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision imetoa
msaada wa vifaa vya kupimia macho wa zaidi ya sh milioni 11.4 kwa Wilaya za
Mkuranga na Kibaha ziliyopo mkoani Pwani mwishoni mwa wiki.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa msada huo ,Kaimu Mkurugenzi wa
Wilaya hiyo Benjamin Majoya alisema msaada huo utasaidia
katika kupandisha kiwango cha taaluma kwa wanafunzi katika
Wilaya hiyo kutokana na idadi ya watoro darasani
kupungua kuanzia mwaka huu.
Alisema kupungua kwa idadi ya wanafunzi watoro kutakwenda sambamba na
kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi watakaojiunga na elimu
yasekondari mwaka ujao.
Majoya alisema msaada uliotolewa na Taasisi hiyo umekuja kwa
wakati mwafaka kwa wakati amabo ulikuwa ukihitajika hivyo mbali ya
kuwasaidia wanafunzi wa shule za msingi lakini pia utawasaidia wananchi
wote wa Wilaya hiyo.
Alibainisha kuwa msaada huo unaojumuisha mashine zote za kupimia
macho pamoja kutengenezea miwani za aina mbalimbali utasaidia
kuondoa tatizo la uoni hafifu ambalo hapo awali wazazi walikuwa na imani potofu
kwamba huenda watoto wao wamerogwa .
Akielezea ukubwa wa tatizo hilo ,alisema kuwa uoni hafifu umekuwa
sababu ya mwanafunzi kutokufanya vizuri kitaaluma kutokana na kuugua mara kwa
mara hivyo kusababisha utoro.
“Tunaishukuru sana Taasisi ya BrienHolden Vision kwa msaada
waliotupatia na tunaahidi kuutumia kwaajili ya wananchi ,na ifahamikie
kwamba hii itabaki kuwa mali ya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
’”alihitimisha Majoya.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Eden Mashayo
alisema lengo la Taasisi yake ni kuwajengea uwezo wa kuona
wanafunzi pamoja na walimu lakini pia kutoa mafunzo kwaajili ya walimu
ili waweze kuwapima wanafunzi wapate huduma stahiki ili kuondokana na
tatizo hilo..
Mashayo aliahidi ushirikiano baina ya Taasisi yake ,Wizara ya
Afya,Wilaya ya mkuranga na kwa kuleta mtaalamu wa masuala ya macho kila
mwezi mara mbili ambaye atakuwa akiwahudumia wakazi wa eneo hilo ili kuondokana
na tatizo la uoni hafifu ambalo litapungua kwa asilimia 10 .
Kwa upande wake Mkuu wa Mratibu wa huduma za macho Taifa
kutoka Wizara ya Afya Dk Nkundwe Mwakyusa alisema kuwa mradi huo
unaosaidia shule za Msingi bagamoyo na Kibaha umeshahudumia shule
121 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili utahudumia shule 116 .
Akizungumzia changamoto zinazowakabili alisema kuwa huduma
hizo hazipewi kipaumbele kwasababu serikali inajua tu kunawafadhili .
Hata hivyo alibainisha kuwa ili kutatuua changamoto hizo na
kuifanya jamii iwe na uelewa sahihi juu ya magonjwa ya macho mikakati
iliyopo huenda mambo yakabadilika na mwaka huu jamii itaanza kupata
taarifa sahihi kuhusu magonjwa ya macho.
Naye daktari Mtalamu wa macho Gilbert Massawe wa hospitali
ya wilaya ya Mkuranga na Afisa Maendeleo ya jamii mji wa kibaha Leah Rwanji
waliishukuru Wizara ya Afya sambamba na Taasisi ya
Brien Holden Vision kwa msaada wao na kubainisha kuwa
utasaidia kupunguza idadi ya utoro kwa wanafunzi kwa asilimia 10.
0 comments:
Post a Comment