Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge(wa kwanza)
akishuka ngazi baada ya kukagua kivuko
cha MV-Utete ambacho hakitoi huduma ya usafirishaji kutokana na kupungua kwa
kina cha maji cha mto Rufiji.
*******
Naibu waziri wa ujenzi,
Eng.Gerson Lwenge ameagiza Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA), kuandaa mpango mkakati wa haraka utakaowezesha
kupatikana kwa kivuko kidogo kitakachotoa huduma katika mji wa Utete wilayani Rufiji.
Hatua hiyo inafuatia
mabadiliko ya tabia nchi yaliosababisha kina cha maji ya mto Rufiji kupungua na
kusababisha kivuko kikubwa cha Mv. Utete kushindwa kufanya kazi kutokana na
upungufu wa maji katika mto Rufiji.
Akizungumza mara baada ya
kukikagua kivuko cha Mv-Utete naibu waziri Eng.Gerson Lwenge amesisitiza hatua za haraka za kuhakikisha
kivuko kidogo kinapatikana ili kutoa huduma kwa wananchi katika kipindi kifupi
na kuondoa usumbufu unaowakabili wananchi kwa sasa.
“Nawapa wiki mbili kuhakikisha
mnapata ufumbuzi wa kivuko kinachofaa kutumika katika mazingira ya mto Rufiji
ili kukiondoa kivuko cha Mv- Utete na kukipeleka mahali pengine ambapo kitaweza
kutoa huduma kikamilifu kuliko kukiacha hapa kikiwa kizima lakini hakitoi
huduma”, amesisitiza naibu waziri Eng. Lwenge.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge (wa pili
kulia) akitoa maagizo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA),
Manase Ole-Kujan baada ya kukagua kivuko
cha Mv-Utete wilayani Rufiji mkoani Pwani juzi.
Kivuko cha MV-Utete ambacho kimeegeshwa na kusitisha huduma zake
kutokana na kupungua kwa kina cha maji cha mto rufiji mkoani Pwani
Naibu Waziri wa Ujenzi
Eng. Gerson Lwenge (wa kwanza kulia) akimpa pole Mkuu wa mkoa wa Pwani Eng. Evarist
Ndikilo kufuatia mauaji ya askari polisi wawili katika kituo cha polisi cha
Ikwiriri Wilayani Rufiji.
0 comments:
Post a Comment