Nafasi Ya Matangazo

December 03, 2014

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya miaka 70 ya Usafiri wa anga duniani yanayoendelea nchini na namna Serikali kupitia Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) ilivyojipanga kuhakikisha usalama wa ndege na abiria wanaotumia anga la Tanzania.
 Afisa mwongoza ndege wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere  Bi. Mossy Kitangita (kulia) akimweleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka  namna kitengo cha uongozaji wa ndege katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kinavyofanya kazi na changamoto wanazokabiliana nazo.
Mkuu wa masuala ya Ulinzi na Usalama katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Bw. Ole Laputi (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la maonesho la idara hiyo kuhusu baadhi ya vimiminika visivyoruhusiwa kwa abiria wanaotumia usafiri wa anga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka (Kushoto) akitembelea banda la maonesho la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kuona  utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu na viwanja vya ndege  katika maeneo mbalimbali nchini.
Posted by MROKI On Wednesday, December 03, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo