Naibu
Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Mhe Stephen Masele
(aliyesimama katikati na pama) akishuhudia halfa fupi ya kusaini
makabidhiano ya eneo la Mgodi wa Resolute kwa Chuo cha Madini Dodoma. Wa
kwanza kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Madini
Dodoma, Mjiolojia Mwandamizi Subian Chiragwile, katikati ni Kaimu
Kamishna wa Madini Mhandisi Ally Samaje, na kushoto ni Meneja Mkuu wa
Mgodi wa Resolute Peter Beilby. Wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wilaya
ya Nzega Bintuni Msangi (wa pili kuchoto aliyesimama),Mkurugenzi Kampuni
ya Resolute Rose Aziz na baadhi ya waliohudhuria.
Meneja Mazingira baada
Mgodi wa Resolute Jackie Sinclair (Kulia), akimkabidhi funguo
mbalimbali za majengo ya eneo la mgodi wa Resolute Naibu Waziri wa
Nishati na Madini (Madini) Stephen Masele (Kushoto) mara makabidhiano ya eneo la mgodi.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele (kushoto) akimkabidhi Mkuu
wa Chuo cha Madini Dodoma Mjiolojia Mwandamizi Subian Chirangilwe funguo
mbalimbali za majengo ya mgodi wa Resolute kwa ajili ya Chuo cha Madini
Dodoma
*******
Na Asteria Muhozya, Nzega
Mgodi
wa Resolute uliopo Wilayani Nzega Mkoani Tabora jana tarehe 12 Desemba,
2014, ulikabidhi eneo la Mgodi kwa Chuo cha Madini Dodoma katika hafla
fupi iliyofanyika na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
anayeshughulikia madini Stephen Masele.
Wengine
walioshuhudia ni, Mkuu wa Wilaya ya Nzega aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa
huo, Mhe. Bituni Msangi, Viongozi Waandamizi wa Wilaya ya Nzega, Kaimu
Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje, Kamati ya Kitaifa ya
uchimbaji, Uongozi wa Juu wa kampuni ya Resolute na wananchi. Naibu
Waziri Masele alieleza kuwa, tukio la kukabidhiwa eneo hilo la Mgodi kwa
Chuo ni tukio ambalo limefungua ukurasa mwingine kutokana na kwamba
Chuo cha Madini Dodoma kitaiwezesha Tanzania kuzalisha wataalamu zaidi
waliobobea katika tasnia hiyo ambao mchango wao kwa taifa unahitajika
katika kuendeleza sekta ya madini.
“Tunataka
wanafunzi wasome kwa vitendo, hii itawezesha kupata wataalamu
waliobobea. Ni nafasi kwa wanafunzi na Chuo cha Madini kuitumia fursa
hii vizuri. Najua kuna mawazo mchanganyiko ya kupoteza mapato kwa
Halmashauri na mengine ya kupata Chuo lakini, kufunga mgodi ni sehemu ya
Sheria ya madini”, aliongeza Masele.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bintuni Msangi, akizungumza katika
halfa hiyo, alieleza kuwa, Mgodi wa Resolute una historia ya kuwa mgodi
wa kwanza nchini kuzalisha madini ya dhahabu na kuogeza kuwa, ndani ya
kipindi cha miaka 12 cha uhai wa mgodi huo umeweza kuchangia kiasi cha
shilingi bilioni 290 za Kitanzania ikiwa ni kodi mbalimbali
zilizotolewa na mgodi huo kama mrahaba.
Aliongeza
kuwa, Halmashauri iliweza kupata kiasi cha shilingi bilioni 6 ikiwa
ni kodi na kiasi cha Tsh bilioni 6 kilitumiwa na mgodi huo kuwezesha za
kijamii ikiwemo ujenzi wa zahanati, shule, upatikanaji wa huduma safi
ya maji katika eneo linalozunguka mgodi huo.
Pamoja
na eneo la mgodi huo kukabidhiwa kwa Chuo cha Madini Dodoma, vilevile
mgodi umekabidhi majengo, mitambo, maabara ambapo, kwa mujibu wa Mkuu
wa Chuo cha Madinini Dodoma, Mjiolojia Mwandamizi Subian Chiragwile
alieleza kuwa, eneo hilo litatumiwa na wanafunzi wa mwaka wa pili kwa
ajili ya masomo ya vitendo.
Mgodi
wa Resolute umefunga rasmi shughuli zake za uchimbaji madini ya dhahabu
katika eneo hilo, ambapo ulianza kazi zake mwaka 1998. Kabla ya
makabidhiano hayo, mgodi huo umefanya ukarabati, ujenzi wa madarasa, na
uhifadhi wa mazingira.
Sehemu mgodi
ambao shughuli za uchimbaji zilikuwa zikifanywa na mgodi wa Resolute
ambao pia umekabidhiwa kwa Chuo cha Madini Dodoma. Kwa mujibu wa Mkuu wa
Chuo Madini Dodoma Mjiolojia Mwandamizi Subian Chirangilwe ameeleza kuwa,mgodi huo utatoa fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa vitendo kuhusu shughuli za uchumbaji.
0 comments:
Post a Comment