Safu
ya waimbaji wa Bendi ya Msondo Ngoma ikiongozwa na Nguli Shaaban Dede
(katikati) wakifanya vitu vya mbele ya mashabiki wao lukuki waliofika
kwenye Viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar.
Bendi
Kongwe ya Muziki wa Dansi hapa nchini iliyodumu kwa miaka 50 toka
kuanzishwa kwake mwaka 1964,Msondo Ngoma Music Band imesherehekea
jubilei yake hiyo iliyofanyika Novemba 1,2014 katika viwanja vya TCC
Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha mashabiki wake
lukuki kutoka sehemu mbali mbali.
Mgeni
Rasmi katika Sherehe hizo ya kusherehekea Jubilei ya miaka 50 ya Bendi
ya Msondo Ngoma,alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye
aliweza kuwatunuku vyeti vya heshima wanamuziki mbali mbali walioitumia
Bendi hiyo toka ilipoanzishwa mpaka sasa.
Mpiga Tumba wa Msondo Ngoma akifanya yake.
Hassan
Moshi William (mtoto wa Marehemu TX Moshi Willian) akionyesha uhodari
wake kiasi kwamba hata pengo la mzee wake kuhisi limezibwa.
Rapa wa Bendi ya Msondo Ngoma,Roman Mng'ande akifanya mambo.
Baba la Mababa,Mzee Said Mabela akiendeendelea kuzikonga nyoyo za Mashabiki wa Msondo.
Abdul Ridhwan "Panga mawe"
KUONA PICHA ZAIDI BOFYA FATHER KIDEVU MATUKIO
0 comments:
Post a Comment