Nafasi Ya Matangazo

November 28, 2014

Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) leo kimefanya mahafali yake ya 40 tangu kuanzishwa kwake huku mgeni rasmi akiwa ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima ambaye alimwakilisha Waziri wake Saada Mkuya. 

Wanachuo hao wamehitimu hii leo huku wengi wao wakiwa na changamoto kubwa ya ajira kufuatia soko la ajira kuwa finyu na wahitimu wengi kuhitaji kazi za kuajiriwa maofisini badala ya kujiari katika njanja mbalimbali ambazo wamezisomea na kupata taaluma. Mahafali hayo yalifanyika katika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam.
Wahitimu walio wengi ni vijana ambao kama wataamua kujiunga katika vikundi na kuanzisha taasisi zao wanaweza kujikwamua katika janga la kutafuta ajira za maofisini. 
 Wahitimu mbalimbali wakiwa katika viwanja vya karimjee Dar es Salaam hii leo katika mahafali hayo.
Wahitimu wa Shahada ya Sayansi katika Bima  na kuzuia majanga wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wakiwa katika picha ya pamoja na mwanafunzi bora wa kozi hiyo, Witness Michael (katikati) aliyetunukiwa cheti kwa kuwa mwanafunzi bora. Wengine ni Aisha Said (kulia) na Rehema Alfonce. IFM ilifanya mahafali yake Dar es Salaam
Posted by MROKI On Friday, November 28, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo