Upepo mkali uliotangazwa na Malka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA) kuwa utakuwa mkubwa na mawimbi bahari ya Hindi umeanza kuleta athari jijini Dar es Salaam kwa miti kuanguka ambapo leo majira ya saa sita mti wa Mnazi mali ya Masjidi Mwenyeheri uliopo kando kando ya barabara ya bibi Titi katika mtaa wa Zanaki kukatika na kuangukia barabarani na kusababisha magari kushindwa kupita kwa muda.
Father Kidevu Blog ilishuhudia Askari Polisi waliokuwa wakipita na gari la doria PT 1145 wakisaiduiana na wananchi kuufunga katika gari hilo na kuusogeza pembeni ili kuruhusu magari kupita kama kawaida.
Baadhi ya wananchi walihoji uharaka wa watu wa jiji katika kuondoa vitu kama hivyo kwa haraka tofauti na wanavyoweza kukamata mama ntilie na wauza mitumba mitaani au kukamata magari yaliyoegeshwa pasipo hitajika na kusahau majukumu yao mengine kama hayo.
Upepo huo pia uliangusha uzio katika kiwanja cha kilichopo makutano ya mtaa wa Samora na Mkwepu Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment