Na Fadha Kidevu Blog
BAADA ya kuibuka na ushindi
kiduchu dhidi ya Thika United ya Kenya kocha wa Yanga, Mbrazili Marcio Maximo amekitetea kikosi chake
kwa kusema mbinu na mfumo anavyotaka kuvitumia kwenye ligi ndiyo vilivyo
changia timu hiyo kuonyesha kiwango cha chini kwenye mchezo wa jana.
Maximo alisema pamoja na
matokeo hayo lakini amewataka mashabiki wa timu hiyo kuondoa hofu na kuwaahidi
kulimaliza tatizo hilo kabla ya kuanza kwa ligi kuu Tanzania bara Septemba 20
mwaka huu.
“Tatizo hili limetokana na
mfumo ambao nimekuwa nikiufundisha ili tuweze kuutumia kwenye ligi siyo kitu
rahisi kuma watu wanavyo fikiria lakini nitahakikisha tunatumia vizuri siku
zilizobaki kabla ya kuanza kwa ligi ili waweze kuushika na kuufanyia kazi
vizuri alisema Maximo.
Yanga keshokutwa Jumapili
inatarajia kushukatena uwanja wa taifa Dar es Salaam,kupambana na mabingwa wa
Kenya Gor Mahia ukiwa ni mchezo wa mwisho wa kirafiki kabla ya kupambana na
Azam kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii Septemba 14 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment