Profesa Pais (kulia), akizungumza na madaktari viongozi na madaktari wa Hospitali ya Bugando. Kutoka kushoto ni Daktari wa Kitengo cha Magonjwa ya Saratani wa hospitali
hiyo Dk.Beda Likonda na Respicius Didace aliyeongoza na msafara wa
Profesa Pais.
Profesa Pais (wa pili kulia), akizungumza na madaktari ha wa Hospitali ya Misheni ya Sengeremao. Kutoka kushoto ni Ofisa Msaidizi wa Muuguzi Mkuu wa hospitali hiyo Daniel Mihayo, Mganga wa hospitali hiyo, Chacha Ernest, Dk.Fred Limbanga ambaye yupo katika msafara wa Profesa Pais na Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira na Respicius Didace. Profesa Pais yupo nchini kwa ziara
maalumu ya kufanya mazungumzo na wadau wa sekta ya afya kuona
uwezekano wa kujenga kituo cha uchunguzi wa ugonjwa wa saratani ya
matiti kwa mualiko wa James Rugemalira.
Ofisa Mawasiliano wa Kimataifa na Maendeleo wa Hospitali
ya Bugando, Josephine Mkono (kulia), akizungumza na Profesa Pais na ujumbe
wake na madaktari wa hospitali hiyo.
Profesa Pais (wa tatu kushoto), ujumbe aliongoza nao na
madaktari wa kitengo cha ugonjwa wa saratani wa hospitali ya Bugando wakiwa
mbele ya jengo jipya la saratani linaloendelewa kujengwa hospitalini
hapo.
Muuguzi wa Hospitali ya Misheni ya Wilaya ya Sebgerema, Oliver Mathias, akimuhudumia mtoto aliyelazwa kwa matibabu katika hospitali hiyo wakati Profesa Pais alipotembea hospitalini hapo. Kulia ni mama wa mtoto huyo.
Moja ya Jengo la Hospitali ya Misheni ya Wilaya ya Sengerema linavyoonekana.
Jengo jipya la saratani linalojengwa katika Hospitali ya Bugando linavyooneka.
Jengo la Hospitali ya Bugando linavyoonekana kwa mbele.
****
****
Na Habari za jamii.com.
DAKTARI bingwa wa ugonjwa ya saratani ya matiti kutoka Bangarole
India, Profesa Anthony Pais, amewataka madaktari nchini kuunganisha
nguvu kukabiliana na ugonjwa huo ambao umekuwa tishio na unaogharimu
maisha ya watu kwa kiasi kikubwa.
“Ugonjwa huu kwa sasa
unatishia maisha ya binadamu kwa kasi kubwa kuliko ilivyokuwa zamani.
Hivyo juhudi zinahitajika sasa kuukabili bila kuchelewa,”
Pais
alisema hayo jana alipokuwa akiongea na madaktari na viongozi wengine
wa Hospitali ya Rufaa ya Bungando Jijini Mwanza.
Amesema kuwa yeye yuko tayari kuanzisha mchakato wa ushirikiano huo ili
kutimiza ndoto yake ya muda mrefu kuona kuwa wagonjwa wa saratani
wanatibiwa hapa nchini badala ya kusafirishwa kwenda India kufuata
matibabu hayo kwa gharama kubwa.
Daktari huyo bingwa
yupo nchini kutembelea hospitali kadhaa kujionea ukubwa wa tatizo
linalosababishwa na ugonjwa huo wa saratani hapa nchini na kuona
uwezekano wa kujenga kituo cha uchunguzi wa ugonjwa huo.
Ziara hiyo inadhaminiwa na kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits
Limited, yenye haki pekee ya kusambaza vinywaji cha Windhoek Larger ,
Windhoek Draught na kinywaji kisicho na kilevi cha Climax hapa nchini.
Mshauri
wa Kimataifa wa Kujitegemea wa kampuni hiyo James Rugemalira alieleza
kuwa kampuni yake ilishitushwa na kuenea kwa ugonjwa huo kwa kasi hapa
nchini ambapo kila siku watu wanapoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.
Hivyo
alisema kuwa kampuni yake iliona umuhimu wa kufanya kila linalowezekana
kutafuta njia za kukabiliana na ugonjwa huo bila kuchelewa.
Profesa
Pais tayari ametembea Dar es Salaam, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Magonjwa ya Saratani ya
Ocean Road, Dodoma, Singida, Kahama, Hospitali ya Wilaya ya Biharamulo,
Hospitali ya Misheni ya Kagondo, Bukoba ambapo alizungumza na wadau
mbalimbali wa sekta ya afya, wakiwemo wanachama wa klabu ya Rotary ya
mkoa wa Bukoba, kuhusu mchakato huo wa ujenzi wa kituo cha uchunguzi wa
saratani ya matiti hapa nchini.
Naye Mkuu wa kitengo
cha magonjwa ya saratani katika hospitali hiyo, Dk. Nestory Masalu,
alimshukuru daktari huyo kutoka India kwa kubuni wazo hilo kwa madaktari
kuunganisha nguvu, kwani ndiyo itakayo kuwa njia pekee ya kupambana na
ugonjwa huo unaogharibu maisha ya watu kila kukicha.
0 comments:
Post a Comment