Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa
mbunge mchungaji Msigwa kushoto akiwa na mbunge Chiku Abwao katika moja kati ya vikao vya baraza la madiwani Manispaa ya Iringa
**********
Na Francis GodwingaBlog
KAMATI ya uchaguzi wa mkuu wa wilaya ya Iringa mjini kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) imemuengua katika kinyang'anyiro cha uenyekiti wa wilaya hiyo mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa ambae ndie alikuwa wenyekiti anayemaliza muda wake kwa kukosa sifa ya kutetea tena nafasi hiyo.
Hatua hiyo ya kuenguliwa kwa Msigwa imekuja baada ya wajumbe kulalamikia hatua ya chama kushindwa kulipa kodi ya ofisi ya kata na ile ya wilaya pia ugomvi mkubwa uliopo kati ya mbunge Msigwa na mbunge mwenzake wa viti maalum mkoa Chiku Abwao aliyekuwa akigombea nafasi ya kiti mkoa wa Iringa nafasi ambayo msigwa pia alitangaza kugombea .
Hivyo kutokana na mvutano huo kamati hiyo iliyoketi usiku wa leo ukumbi wa Sambala mjini hapa ililazimika kuchukua uamuzi mgumu wa kufyeka majina ya wabunge hao kugombea nafasi hizo ili kunusuru chama.
Mmoja kati ya makada wa ambae alishiriki kikao hicho cha kumuengua Msigwa na Chiku alisema kuwa chanzo cha msigwa kuenguliwa ni kutokana na kuendekeza kukuza makundi ndani ya chama na kuwa mbali na chama zaidi ya kufanya chama kuendelea kukosa heshima.
Makundi hayo yanaelezwa kukiwekwa rehani chama hicho wakati kikijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Pamoja na Mchungaji Msigwa, taarifa hizo zimesema Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Chiku Abwao (Chadema) naye ameenguliwa kuwani nafasi yoyote ya uongozi katika chama hicho mkoani hapa.
Hivikaribuni Abwao alinukuliwa akitangaza kuwania nafasi ya uenyekiti wa mkoa wa chama hicho unaotarajia kufanyika Jumapili keshokutwa.
Kuenguliwa kwa Msigwa katika uchaguzi huo kumeacha kampuni wagombea wawili wanaomenyana katika nafasi hiyo itakayosaidia kutoa picha ya jinsi mambo yatakavyokuwa wakati wa mchakato wa kumpata mgombea ubunge jimbo la Iringa Mjini mwaka 2015.
Wagombea hao ni Frank Nyalusi anayeelezwa kuwa ni mfuasi wa kufa na kupona wa Mchungaji Peter Msigwa na Mohamed Makuke ambaye ni mfuasi wa kundi la wengi linalodaiwa kumpinga Mchunngaji Msigwa.
Kundi linalojiita la wengi katika chama hicho limesikika likisema mara kwa mra kwamba tabia ya Mchungaji Msigwa ndani ya chama hicho inawaweka katika wakati mgumu wa kutetea nafasi ya ubunge mwaka 2015.
Mchungaji Msigwa ni kiongozi asiyeambilika, anayejua kila kitu, mbishi, kaidi, mwenye kiburi, asiyependa watu, mwenye visasi, majivuno na asiyetaka ushirikiano toka kwa wenzake, asiye na mikakati ya kujenga chama huku akiamini siasa za kitaifa pekee anazopenda zaidi zinaweza kulinusuru jimbo hili katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani.
Wakati Mchungaji Msigwa akirushiwa lawama zote hizo, taarifa za uhakika zimedai kwamba ofisi ya wilaya ya chama hicho imefungwa na wameamuliwa kuondoka baada ya uongozi wa mbunge huyo unaomaliza muda wake kushindwa kulipa kodi ya pango. Mchungaji Msigwa ndiye Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Iringa Mjini anayemaliza muda wake hii leo.
Wanachama wa chama hicho wamechukizwa kwa hatua ya mbunge wao kuridhia kupoteza ofisi pekee ya chama hicho mjini Iringa kwasababu ya kushindwa kulipa Sh 540,000 walizokuwa wakidaiwa.
Kwa upande wake mbunge Msigwa alinukuliwa na mwandishi wa habari hizi akimrushia maneno mmoja kati ya viongozi wa chama hicho kuwa watu wanamchafua kwa suala la ofisi na kuwa ni ruksa kwa wanachama ambao wanapenda vyama vyenye ofisi kuhama chadema na kujiunga na vyama hivyo.
Huku mbunge Chiku Abwao amethibitisha kuenguliwa kwao katika nafasi hizo japo amedai kwa upande wake kaonewa na ataendelea kutumia vikao kuomba kurejeshwa kwa jina lake.
0 comments:
Post a Comment