WAZIRI WA mali asili na Utalii, Lazaro Nyalandu (pichani) ametangaza
rasmi kuifutia leseni ya uwindaji nchini pamoja na kuifuta kabisa kampuni hiyo
katika shughuli za utalii nchini Kampuni ya Uwindaji Green Miles Safaris Limited (GMS) kutokana na kukiuka sheria mbalimbali za
uwindaji Wanyamapori.
Nyalandu ametangaza uamuzi huo leo mchana jijini
Dar es Salaam, kutokana na kuridhishwa
na ushahidi kuhusu kampuni hiyo kufanya vitendo vya kuwatesa wanyama pori.
Kampuni ya “Green Miles Safaris Limited(GMS) ililalamikiwa
kwa mara ya kwanza na Mbunge Iringa mjini ambaye pia ni Waziri Kivuli wa
Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa, Bungeni mjini Dodoma wakati
akiwasilisha bajeti kivuli ya wizara hiyo ambapo katika ushahidi wake
aliwasilisha na CD ambazo zilikuwa na matukio hayo.
GMS ilituhumiwa kuendesha uwindaji haramu
ikiwamo kujeruhi wanyama, kuuwa wanyama wa jinsi ya kike, kuchezea watoto wa
Pundamilia, mtoto akiwinda na kuua ndege aina tandawala weupe na weusi na
matumizi ya silaha zisizo na sauti.
Green
Miles Safaris Limited, inamilikiwa na Mtanzania, Salum Awadh.
0 comments:
Post a Comment