Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine (kushoto),
akikabidhi Shs. milioni 5 kwa Mwenyekiti wa Vikoba Kata ya Engutoto, Bilhuda
Kisasa, ikiwa ni sehemu ya mchango wake
wa shs. milioni 10 alizoahidi kuwasaidia akinamama wa kata hiyo.
Mbunge
wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine (kulia), akizindua katiba ya
vikundi vya vikoba katika kata ya Engutoto Wilayani Monduli jana. Hafla hiyo
ilikwenda sambamba na harambee ya kutunisha mfuko wa vikoba, ambapo katika
harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 12 zilipatikana. Kushoto ni Mwenyekiti
wa vikoba kata ya Engutoto, Bilhuda Kisasa .
Mbunge
wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine (kulia), akizindua katiba ya
vikundi vya vikoba katika kata ya Engutoto Wilayani Monduli jana. Hafla hiyo
ilikwenda sambamba na harambee ya kutunisha mfuko wa vikoba, ambapo katika
harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 12 zilipatikana. Kushoto ni Mwenyekiti
wa vikoba kata ya Engutoto, Bilhuda Kisasa .
********
NA MWANDISHI WETU, ARUSHA
WANACHAMA wa vikundi vya kuweka na
kukopa (VIKOBA) mkoani Arusha wametakiwa kutumia na kupanga vizuri matumizi ya
fedha wanazokusanya ili ziwasaidie kutoka daraja mhadi jingine katika maisha
yao.
Kauli hiyo ilitolewa jana wilayani
hapa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha Namelok Sokoine alipokuwa
akiendesha utunishaji wa fedha kwa Umoja wa Wanavikoba wa Kata ya Engutoto
yenye vikundi 20 na wanachama 600.
Katika utunishaji huo, Namelok
alichangia Sh. Milioni 10 huku kiasi cha Sh. Milioni 12 kikipatikana katika
shughuli hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Umoja wa Wanawake UTW
wilayani Monduli.
Akizungumza na wanavikundi hao Mbunge
Namelok aliwataka wanawake kujitokeza na kujiunga katika vikundi huku akiwataka
kuacha kuogopa kufanya shughuli za ujasiriamali.
“Wanawake nawaomba sana muendelee
kujitokeza na kujiunga katika Vikoba kwani huku ndipo eneo ambalo litatuwezesha
tuwe na sauti ya kujitegemea kimapato.
“Lakini pia naomba niwakumbushe jambo
muhimu hizi fedha tunazokusanya nawaomba sana muonyeshe mfano wa kuzitumia
vizuri ili kesho zitusaidie kutoka daraja moja kwenda daraja jingine katika
maisha yetu,” alisema Namelok.
Kwa upande wake Katibu wa UWT Kata ya
Engutoto Glory Emmanuel alisema wana vikundi wengi waliopo kwenye vikoba
wanakabiliwa na changamoto ya elimu ya ujasiriamali.
“Tunaomba suala la ofisi za vikoba
uliangalie kwani vikundi havina ofisini.Pia wanachama hawana elimu hatua
inayosababisha kukopa na kutumia sivyo kutokana na kutokuwa na elimu ndogo ya
biashara,” alisema Glory.
Naye mwana kikundi Zaituni Mwishehe
alibainisha jinsi alivyonufaika na kuwa katika vikundi hivyo vya kuweka na
kukopa ambapo hadi sasa ameweza kujitegemea katika matumizi ya kawaida ndani ya
nyumba.
“Sasa hivi naweza kulipia michango
midogomidogo ya mwanangu shuleni. Lakini pia hata kutatua matatizo mengine ya
kifamilia kupitia mikopo ninayochukua kwenye kikundi bila hata kumsubiria mume
wangu,” alisema Zaituni.
0 comments:
Post a Comment