Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema kuwa
tume hiyo haiendeshwi na rimonti kwani ni chombo kinachojitegemea katika
kufanya shughuli zake hivyo amewaasa wananchi na wanasiasa kuondoa
fikra potofu juu ya tume hiyo.
Pia Jaji
Lubuva ameongeza kuwa tume hiyo haifanyi kazi kwa kushinikizwa na mtu
yeyote Yule badala yake wanafanya kazi kutimiza jukumu walilopewa
kitaifa.
Aliyasema
hayo jana jijini Arusha
wakati akitambulisha mfumo mpya wa kuboresha daftari la kupigia kura
kwa kutumia teknolojia ya Biometric Voter Registration (BVR) ,ambapo
alisema kuwa teknolojia hiyo itaanza kutumika mwezi Agusti
mwaka huu katika shughuli za uboreshaji wa daftari la wapiga kura
Aidha alisema kuwa mfumo huo utaleta maboresho na utasaidia kuwepo kwa daftari la kura linaloeleweka na lisilo na mashaka.
Pia aliongeza kuwa siku 14 za wananchi kufika
katika vituo vya kupigia
kura kuboresha taarifa zao na kuandikisha wapiga kura wapya ambao
hawaklupata fursa hiyo na kuwa zoezi hili litawahusu Watanzania wote.
Kuhusiana
na matukio ya mabomu yanayojitokeza hususani Mkoa wa Arusha alisema
kuwa ulinzi utaimarishwa ili kuwapa fursa wananchi kujitokeza kupiga
kura kwa usalama
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela amesema kuwa
maboresho hayo yatasaidia ushiriki mpana wa wananchi katika kutimiza
haki zao za kidemokrasia na kikatiba za kupiga kura hivyo amewaomba
wananchi wajitokeze kwa wingi katika zoezi hilo
.(Pamela Mollel jamiiblog)
.(Pamela Mollel jamiiblog)
0 comments:
Post a Comment