MenejawaBiaya Safari Lager,
Oscar Shelukindo(kulia) akimkabidhiMwenyekitiwa Chama cha Pool Taifa,
IsacTogochokikombe cha bingwawamashindanoya Pool Taifayajulikanayokama “Safari
National Pool Competition 2014” wakatiwauzinduziwamashindanohayouliofanyika TBL
Dar es Salaam leo.KatikatiniKatibuwa cha hicho, Amos Kafwinga.
MenejawaBiaya Safari Lager,
Oscar Shelukindo(kulia) akimkabidhiMwenyekitiwa Chama cha Pool Taifa,
IsacTogocho ngao ya mshind iwa kwanza mmojammoja wamashindanoya Pool Taifayajulikanayokama
“Safari National Pool Competition 2014”
wakatiwauzinduziwamashindanohayouliofanyika TBL Dar es Salaam
leo.KatikatiniKatibuwa cha hicho, Amos Kafwinga.
Katibuwachama cha Pool Taifa,
Amos Kafwinga (kushoto) akichezawakatiwauzinduziwamashindanoya Pool Taifayajulikanayokama
“Safari National Pool Competition 2014”yaliyofanyika TBL Dar es Salaam
leo.KulianiMwenyekitiwa TAPA, IsacTogochonaMenejawaBiaya Safari Lager, Oscar
Shelukindo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa bia ya Safari Lager
, Oscar Shelukindo amesema kuwa mwaka huu wameamua kuboresha mashindano ili kuongeza hamasa na changamoto kwa vilabu kwa kuongeza zawadi asilimia 15% .
Shelukindo alisema jumla
ya Sh.Mil.86 zimetengwa kwa ajili ya
mashindano hayo kwa mwaka wa 2014.
Bingwa wa kila mkoa kwa upande wa timu atapata Sh.800,000 kutoka
Sh.500,000 ya msimu uliopita, mshindi wa pili Sh.400,000, mshindi wa tatu
Sh.250,000.
Shelukindo alisema kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume),
bingwa atapata Sh.400,000, mshindi wa pili Sh.250,000, wakati bingwa kwa upande
wa mchezaji mmoja mmoja (wanawake), atapewa Sh.300,000 na mshindi wa pili
Sh.200,000.
Mashindano ya mchezo wa
pool ya ‘Safari Lager National Pool Championship 2014’, ngazi ya mikoa
yanatarajia kuanza Juni 14, mwaka huu katika mikoa 18 ya Tanzania Bara.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam,
katibu mkuu wa chama cha mchezo huo taifa (TAPA), Amosi Kafwinga alisema
mashindano hayo yatafikia yatamalizika Septemba 14, mwaka huu.
Kafwinga alisema fainali za taifa za mashindano hayo
yanayodhaminiwa na wadhamini wakuu wa mchezo huo nchini, Kampuni ya Bia Tanzania(TBL)
kupitia bia ya Safari Lager, ambazo zitashirikisha mabingwa wa kila mkoa,
zitafanyikia mkoani Kilimanjaro.
Aliongeza kwa kuitaja mikoa itakayoshiriki mashindano hayo kuwa ni
pamoja na mikoa maalum ya kimichezo ya Kinondoni, Ilala, Temeke, Pwani,
Marogoro, Dodoma, Tanga, Lindi, Manyara, Mbeya, Kilimanjaro, Arusha, Tabora,
Shinyanga, Mwanza, Kagera na Iringa.
0 comments:
Post a Comment