Nafasi Ya Matangazo

May 27, 2014

Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Finland nchini Mhe Sinikka Antilla alipokutana naye Ikulu Dar es salaam leo Mei 27, 2014.

Balozi Antila ndiye Mwenyekiti wa Kundi la Nchi 12 Washirika wa Maendeleo zinazosaidia bajeti ya Tanzania (General Budget Support Group), na amechukua nafasi hiyo tangu mwezi April mwaka huu.

Lengo la Balozi Antila  kuonana na Katibu Mkuu Kiongozi ni kujitambulisha kwa wadhifa huo mpya na kueleza jinsi atavyotekeleza jukumu hilo la Uenyekiti. Pia ameelezea vipaumbele walivyojiwekea katika kuchangia bajeti ya serikali na wakabadilishana mawazo ya namna ya kuimarisha mjadala (dialogue) kati ya kundi hilo la nchi washirika wa maendeleo na Tanzania.
Posted by MROKI On Tuesday, May 27, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo