Nafasi Ya Matangazo

May 05, 2014

 Afisa mtendaji Mkuu Airtel Africa Christophe Soulet akikata utepe kuzindua duka la  Airtel lililopo mlimani city  jijini Dar es Saalam.wakishuhidia,wapili ni Andre Beyers Afisa mkuu wa masoko Airtel Afrika akiwa na meneja wa duka Wahida Saleh na Adriana Lyamba Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Tanzaania
Afisa mtendaji Mkuu Airtel Africa Christophe Soulet akikata utepe kuzindua duka la  Airtel  lililopo mlimani city  jijini Dar es Saalam.wakishuhidia,wapili ni Andre Beyers Afisa mkuu wa masoko Airtel Afrika akiwa na meneja wa duka Wahida Saleh na Sunil Colaso Mkurugenzi Mkuu Airtel Tanzania.

Airtel Tanzania mwishoni mwa wiki hii imezindua duka la Mlimani City baada ya kulifanyiwa  matengenezo na kulipatia sura ya kisasa zaidi. Uzinduzi huu ni kielelezo cha kampuni hiyo  kutoa huduma bora za simu kwa wateja wake.

 Akiongea wakati wa uzinduzi Christophe Soulet, Afisa Mtendaji Mkuu Africa alisema” Airtel tunaamini katika kutoa huduma bora za kisasa zinazoendana na mahitaji ya wateja wetu huku tukiwapa uzoefu wa pekee katika hudumazetu.  Mpango huu wa kuboresha maduka yetu unafanyika katika masoko yetu yote yaliyoko barani Afrika na Leo ninayofuraha kuzindua duka hili la kisasa lijulikanalo kama Express shop hapa nchini Tanzania. 

Duka hili la kisasa linathibitisha  dhamira yetu ya kutoa huduma bora Tanzania na Afrika kwa ujumla
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso  alisema” duka hilo ni la kwanza kuzinduliwa kwani tunabadilisha maduka yetu yote nchi nzima na kuyafanya yawe na mtazamo mpya na wa kisasa zaidi. Duka hili limetengenezwa na kuhakikisha mteja ataweza kupata huduma kwa haraka , kwa usalama bila usumbufu wowote.

Aliongeza kwa kusema Airtel inapenda kuwahakikishia wateja kupata huduma bora wakati wote na pia kupata simu za aina mbalimbali ambazo zitapatikana katika duka hilo jipya la Mlimani City.

Kwa kupitia mtandao wetu mpana ulionea zaidi tunawahakikishia wateja wetu  huduma bora za kisasa, za uhakika jijini Dar es salaam. 

Duka la Mlimani City litaendelea kuuza bidhaa mbalimbali kama vile modem na simu za aina mbalimbali ,  wateja watapata huduma ya Airtel money kwa usalama zaidi , kuunganisha na huduma za simu za malipo ya mwenzi na ya awali , pamoja na huduma za internet na kuunganishwa na mtandao  na kuperuzi kwenye internet , kununua muda wa maongezi pamoja na huduma nyingine nyingi.
Airtel Tanzania inaendele kuboresha huduma zake kwa wateja ambapo inaendele kuboresha maduka yake nchini nzima kwa mwaka huu wa 2014.  Mpango ni kuwafikiwa wateja wengi zaidi na kuboresha huduma zake kupitia maduka yake yote yaliyoko nchi nzima.
Posted by MROKI On Monday, May 05, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo