Nafasi Ya Matangazo

April 03, 2014

Timu nzima ya Tanzania Movie Talents kutoka kampuni ya Proin Promotions Limited wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza safari ya kuelekea Mwanza kwaajili ya shindano la kutafuta Vipaji vya Uigizaji Tanzania ambapo shindano hili litaanzia katika Kanda ya Ziwa katika Mkoa wa Mwanza Kuanzia tarehe 5 April 2014 mahali ni Isamilo Lodge.
Mdau Karimu Muhidin Michuzi na Baadhi ya vijana wa kazi katika timu ya kusaka vipaji wakiwa tayari kwa safari ya Mwanza.
Mabasi yakiwa tayari kwa safari ya Mwanza.
Timu nzima ya Kampuni ya Proin Promotions Limited imeondoka leo jijini Dar Es Salaam kuelekea Mkoani Mwanza kwaajili ya kuendesha Shindano la Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania ambapo Kwa kuanza shindano hili litaanzia Mkoani Mwanza Katika Kanda ya Ziwa.
Usaili wa Kutafuta vipaji utafanyika mnamo tarehe 5 mwezi huu katika ukumbi wa Isamilo lodge ambapo vijana wengi wanaomba kuhudhuria kwa wingi ili kuweza kuonyesha vipaji vyao.
Zoezi la kusaka Vipaji katika Kanda ya ziwa utafanyika kwa Siku nne kuanzia tarehe 5 mwezi huu na pia kwa kanda ya Ziwa Usaili utafanyika katika Mikoa Miwili ya Kigoma na Mwanza.
Proin Promotions Limited imeamua kusaka vipaji ili kuweza kuinua tasnia ya filamu nchini.
Posted by MROKI On Thursday, April 03, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo