LICHA ya kuwa ni kusafisha jiji la Dar es Salaam lakini imeelezwa na wadau mbalimbali hasa wa habari jijini humo kuwa kitendo cha jiji la Dar es salaam kuvunja na kuharibu meza za kuuzia magazeti kwa madai ya kuchafua jiji ni udhalilishaji wa bishara hiyo halali nchini ambayo makampuni yake yanalipa kodi.
Pichani ni mfanya biashara wa magazeti ambaye aliamua kuweka chini magazeti yake eneo la Posta Dar es Salaam baada ya meza yake ya Kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN) wachapaji wa magazeti ya Daily News, Habarileo na Spotileo kuchuliwa na mgambo wa jiji wakati wa operesheni safisha jiji.
Father Kidevu Blog ilizungumza na watu mbalimbali kupata maoni yao juu ya hilo na wengi walisema hatua hiyo ni kudhalilisha biashara ya magazeti.
"Kuzuia uuzaji magazeti jijini Dar es Salaam ni sawa na kuwanyiwa wananchi haki ya kupata habari, hivyo ni ukiukwaji wa sheria za nchi...hawa wauza magazeti ndio wanaturahisishia sisi kupata taarifa mbalimbali.," alisema kazi huyo wa jiji Geofrey Amon.
Aidha pia wameomba makampuni ya magazeti kuungana na kulipigia kelele suala hilo ili wananchi waweze kupta magazeti katika mkaeneo waliyozoea.
Baadhi ya wauzaji hao wa magazeti wamesema biashara hiyo haichafui jiji hivyo waruhusiwe kufanya biashara hiyo bila usumbufu.
Pia zoezi hilo limewakumbwa mafundi viatu wanao safisha viatu na kuvingarisha katika maeneo mbalimbali hasa katikati ya jiji.
0 comments:
Post a Comment