LEO TAIFA la Tanzania linaadhimisha kifo cha Mwanamapinduzi ya Visiwa vya Zanzibar na rais wa Zanzibar ambaye pia alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania, Sheikh Aman Abeid Karume aliyeuwawa kwa risasi mnamo Aprili 7, 1972
na mtu aliyetajwa kuwa ni Luteni Hamud Mohamed Hamud.
Nimiaka 42 tangu mauaji hayo yaliyofanywa na Hamud pia tunaelezwa kuwa alikuwa ni mtoto wa Mzee Mohamed Hamud aliyekuwa mpinzani mkubwa wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na alikamatwa na kuuawa baada ya Mapinduzi ya
Januari 12, 1964 kwa tuhuma za kutaka kuipindua serikali mpya ya Karume.
Hayati Karume aliwawa akiwa na swahiba wake Sheikh Thabit Kombo aliyekuwa Katibu Mkuu wa ASP , walikuwa wote wakicheza bao katika ofizi zao
zilizopo Kisiwandui.
Hakika ni Tukio la majonzi sana kwa Wazanzibari na Tanzania kwa ujumla kwa mauaji hayo. Sote tunaungana kumtakia Pumziko jema Mwanamapinduzi wetu na muasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao leo tunakaribia kuadhimisha miaka yake 50.
0 comments:
Post a Comment