Wakazi
wa eneo la Mapinga Mkoani Pwani wakiwa kwenye mshangao mkubwa baada ya
kushindwa kuvuka Daraja la Mto unaokatisha kwenye eneo hilo baada ya
kutokuwepo kwa mawasiliano ya barabara kwa kukatika kwa daraja hilo
kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa katika maeneo
mbali mbali hapa nchini.
Akithibitisha
kutokea kwa hitilafu hiyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani,ACP Ulrich
Matei amesema ni kweli kumetokea kwa tatizo hilo na amewataka watumiaji
wa barabara ya Bagamoyo kubadilisha njia na kuwanza kutumia barabara ya
Morogoro mpaka hapo daraja hilo litakapofanyiwa matengenezo.
Wakati jitihada zikifanyika kurudisha mawasiliano ya barabara na makamanda wakitafakari juu ya kuweka daraja la muda, watu wameanza lawama eti mkandarasi. Lakini ukweli ni mambo ni matatizo yetu wenyewe. Ukiangalia kati ya hizi picha, kuna moja inaonekana na matete katikati na pembeni yake, kushoto na kulia yanapita maji. Maeneo haya yanayopita maji kwa kipindi fulani yalikuwa yakichimbwa mchanga na kuacha katikati ya mto kuwa na mwinuko. Mvua nyingi maji yamepita pembeni na hata kwenda nje ya daraja.
Mawasiliano kati ya Dar na Bagamoyo kwa barabara ya Bagamoyo yamekatika. Maji yanayopita katika mto Mpigi ambako daraja halipitiki ni mengi sana kiasi kwamba nguzo tatu zinazopitisha umeme mkubwa kwenda Bagamoyo zipo hatarini. Mojawapo maji yanaikaribia zaidi na uwezekano wa kusombwa ni mkubwa kwa sababu miti mikubwa iliyokuwa karibu na eneo hilo nayo imeng'olewa kirahisi kabisa.

0 comments:
Post a Comment