Na Anna Nkinda- Maelezo,
Lindi
Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Taifa (NEC) wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete amewataka wazazi na walimu
kushirikiana kwa pamoja na kuhakikisha wanafunzi wanakwenda shule na kusoma jambo ambalo litasaidia kupanda kwa kiwango
cha elimu mkoani humo.
Mama Kikwete ambaye pia
ni Mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete alitoa rai hiyo hivi karibuni wakati
akiongea na wananchi pamoja na wanafunzi
wa kijiji cha Ruaha waliofika kumsalimia mara baada ya kumaliza mkutano
wake na viongozi wa Halmashauri kuu ya
tawi la Ruaha lililopo katika kata ya Mingoyo
wilaya ya Lindi mjini.
Mjumbe huyo wa
Halmashauri Kuu Taifa alisema kiwango
cha elimu katika mkoa huo kiko chini lakini kama wazazi watahakikisha watoto
wao wanaenda shule kwa wakati na walimu wakihakikisha watoto wamefika shule na kuwafundisha
kiwango cha elimu kitapanda kwa kiasi kikubwa.
“Na ninyi watoto muache
tabia ya kupoteza muda kwa kuokota mabibo au maembe tumieni muda huo kusoma kwa
bidii na kufanya vizuri katika masomo yenu kwa kufanya hivyo mtakuwa na maisha
mazuri hapo baadaye”, alisema Mama Kikwete.
Akiwa katika matawi la
Mkwaya, Ruaha na Majengo Mama Kikwete aliwataka vijana wa CCM kuungana kwa
pamoja na kutafuta eneo kubwa la kikundi
ambalo watalitumia kulima kilimo cha mazao
ya biashara kama vile ufuta ambao utawapatia fedha nyingi na hivyo kujikwamua kiuchumi.
Aidha Mama Kikwete pia
aliwataka kinamama kwenda kupima saratani ya mlango wa kizazi ambayo inauwa
wanake wengi lakini vifo vya ugonjwa huo vinazuilika kama mgonjwa atakwenda
kupima mapema na akigundulika kuwa na dalili za ugonjwa huo katika hatua za
awali ataweza kupata matibabu na kupona.
0 comments:
Post a Comment