KATIBU Mkuu wa zamani
wa Umoja wa Mataifa ya Afrika (OAU, sasa Umoja wa Afrika - AU), Dk. Salim Ahmed
Salim, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika onesho maalum la Usiku wa Mwambao
asilia utakaosindikizwa na bendi za Dar
Modern Taarab na Nadd Ikhwan (Malindi), ndani ya ukumbi wa Travertine, Magomeni
jijini Dar es Salaam, Jumamosi hii April
19
Mlezi wa heshima wa kundi la Dar Modern Taarab, ambaye pia
ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, alisema Dk. Salim ambaye
pia ni Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, amethibitisha kujumuika na wadau na
mashabiki wa taarabu asilia.
Idarous alisema wadau wa muziki wa taarabu watafurahia usiku
huo wa Mwambao Asilia kutoka kwa wanamuziki nguli wa miondoko hiyo Bara na
Visiwani.
“Usiku wa Mwambao Asilia, utasheheni magwiji wakongwe wa
muziki wa taarabu nchini, kutoka kundi la Dar Modern Taarab na Nadd Ikhwan,
ambao wataporomosha nyimbo za taarabu asili za zamani na za sasa,” alisema
Idarous.
Aliongeza kuwa pia usiku huo utapambwa na ‘surprise’,
ikiwemo watu mbalimbali kupita kwenye zulia jekundu ‘red carpet’ na kupiga
picha za ukumbusho na mastaa watakaohudhuria.
Alisema katika usiku huo, kiingilio kitakuwa ni sh 10,000
ambapo tayari tiketi zilishaanza kuuzwa sehemu mbalimbali.
Idarous alizitaja sehemu hizo kuwa ni duka la Fabak
Fashions, Regency Park Hotel Mikocheni na Dar Modern Taarab Hall Magomeni
Ifunda.
Onyesho hilo pia limedhaminiwa na Times FM, Fabak Fashions
na www.nakshi255.com
0 comments:
Post a Comment