Meneja Mwandamizi wa Uhusiano
wa Serikali kutoka Zantel Bw. Charles Jutta (kushoto), akiwakabidhi hundi yenye thamani ya
shilingi milioni 10 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (katikati) na Katibu Mtendaji wa Chama cha
Netiboli Tanzania Bi. Anna Kibira. Fedha hizo ni kwaajili ya
kusaidia Chaneta leo jijini Dar es Salaam
***********
Na Frank Shija - WHVUM
Serikali yapokea msaada wa
shilingi milioni 10 kutoka Zantel kwa lengo la kusaidia Chama cha Netiboli
Tanzania (Chaneta)leo jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa ili kusaidia
katika mashindano ya Netiboli ya Afrika Mashariki na Kati.
Akizungumza wakati wa
makabidhiano wa msaada huu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Bi Sihaba Nkinga ameishukuru kampuni ya Zantel kwa kuonyesha utayari wa kusaidia na
kuendeleza vipaji mbambali katika Nyanja ya michezo.
“Ninaipongeza kampuni ya
Zantel kwa kuonyesha utayari wake katika kusaidia kukuza vipaji vya michezo
hasa katika michezo ya Netiboli, Judo na Ngumi, naamini huu ni mwanzo tu.”
Alisema Bi. Sihaba Nkinga.
Aidha Katibu Mkuu huyo
amewaomba viongozi wa Chaneta kutumia vizuri msaada huo katika kutekeleza
malengo yaliyokusudiwa ili kujenga imani kwa wadau mbambali kuendelea kusaidia
sekta ya michezo
Kwa upande wake Meneja
Mwandamizi wa Uhusiano wa Serikali kutoka Zantel Bw. Charles Jutta amesema kuwa
kampuni yake imeshawishika kutoa msaada huo baada ya kuridhika na utendaji na
muundo wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta)
Aliongeza kuwa msaada huu ni
mwanzo wa Zantel kusaidi sekta ya michezo na kwa kuanzia wamechagua kusaidia
michezo ya Netiboli, Judo na Ngumi na ndiyo maana leo (jana) wanatoa msaada wa
shilingi milioni 10 kwa ajili ya kusaidia mashindano ya netiboli Afrika Mashariki na Kati.
Hata hivyo Jutta amewaomba
wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia ukuzaji vipaji katika michezo mbalimbali
na kusema kuwa ikiachiwa Serikali peke yake haitaweza kufanikisha azma hii
njema ya kufikia mafanikio katika michezo.
Wakati huo huo Katibu Mtendaji
wa Chaneta Bi. Anna Kibira ameishukuru kampuni ya Zantel kwa msaada huo na
kusema kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka ambapo chama chake kimeaanda
mashindano ya kimaataifa.
Kibira aliongeza kuwa
watafanya kila liwezekanalo kuhakikisha msaada huo unazaa matunda na kuleta
sifa kwa taifa kwa kufanikisha mashindano hayo kuwa bora na yenye kukidhi
viwango vya kimataifa.
Mashindano ya mpira wa
Netiboli ya Afrika Mashariki na Kati yatafanyika kuanzia tarehe 22 mwezi
huu(machi)ambapo jumla timu 22 zinatarjiwa kushiriki, kati ya timu hizo timu 10
zinaumdwa na wanaume.
0 comments:
Post a Comment