KITUO cha Uwekezaji
Tanzania (TIC) kimefanikiwa kusajili miradi 9,442 tangu kuanzishwa kwake hadi
2013.
Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano wa TIC, Pendo
Gondwe (pichani juu) wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Gondwe alisema kuwa Watanzania wamekuwa na muamko katika
uwekezaji ambapo katika miradi yote miradi ya Watanzania ni asilimia 52 na 25 ni miradi inayomilikiwa kwa ubia kati
ya wageni na watanzania.
Aliongeza kuwa asilimia 23 ni miradi
iliyowekezwa na wageni kutoka mataifa mbalimbali ambapo alisema miradi ambayo
inaongoza kwa uwekezaji ni Kilimo, Maliasili, Miundombinu, Nishati, viwanda
na biashara, Usafirishaji, Elimu, Afya, Miundo mbinu na madini.
Alisema TIC inawahamasisha Watanzania kujitokeza
kuwekeza katika miradi mbalimbali ili kusaidia katika kukuza uchumi wa Taifa.
Gondwe alisema TIC imekuwa na utaratibu wa
kuhamasisha wananchi kushiriki katika uwekezaji katika sekta nmbalimbali ambapo
kituo hicho kimekuwa kikitumia mikutano na makongamano kuhamasisha wananchi
kusajili miradi yao.
Kituo cha
uwekezaji kinatoa huduma mbalimbali kwa ajili ya wawekezaji wa ndani
kupitia dirisha moja yaani ONE STOP CENTRE ikiwemo kuandikisha kampuni, kujisajili na
VAT, TIN, na leseni mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment