Nafasi Ya Matangazo

March 26, 2014



Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo akizungumza na wana habari wakati wa droo ya saba ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti mara baada ya kuchezesha droo hiyo mapema leo katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bakari Maggid na kushoto kwake ni Afisa Mwandamizi kutoka PWC Golder Kamuzora.
 ********
KAMPUNI ya bia ya Serengeti imeendelea kuchezesha droo zake za winda safari ya Brazil na Serengeti na leo washindi wawili wa simu za kisasa aina ya Samsung galaxy tablet wamepatikana. Kwa mtu kujishindia zawadi zetu unahitaji kununua chupa ya bia ya Serengeti na kuangalia chini ya kizibo ambapo utakuta bia ya bure au tarakimu 6 ambazo utazituma kwa ujumbe mfupi kwenda namba 15317 ambapo utapata ujumbe ukikujulisha kama umejishindia fedha taslimu kati ya shilingi 5000 na shilingi 10000 na pia namba yako itaingizwa katika droo ambapo utaweza kujishiandia king’amuzi, simu ya mkononi au tiketi ya kwenda Brazil.

Mji wa moshi katika maeneo ya majengo umepata bahati ya kutoa washindi wawili wa simu aina ya Samsung tablet. Juma lililopita katika droo ya 6 ya winda safari ya Brazil washindi wawili waliopatikana wote wanatokea katika maeneo ya Majengo Moshi. Droo hiyo ilishuhudiwa na waandishi wa habari, ofisa kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha, PWC pamoja na Push mobile media. Droo kubwa itatoa tiketi ya kwenda Brazil ambaponmshindi atalipiwa gharama zote kwa siku atakazokaa huko.

Meneja wa bia ya Serengeti Bw Rodney Rugambo aliongea na mshindi wa kwanza Bw Matei Kleti Mofulu kutoka Nyakato, Mwanza. Akiwa na furaha muda wote wa maongezi alisema hajaamini kama ameshinda na amekuwa akiamini michezo hii siyo ya ukweli ila Serengeti wamemfumbua macho kuwa ni za kweli. Mshindi wa pili pia alipokea habari hizi kwa furaha na kusema kuwa ni muda kuwa wa kisasa kwa kutumia simu ya kisasa. Pia mshindi wa pili wa simu ya kisasa Bw Godwin Paul ambaye ni mwanajeshi wa JWTZ aliishukuru kampuni ya bia ya Serengeti kwa zawadi hiyo na kuwashauri watumiaji wa Serengeti kushiriki katika promosheni hii.

Tafrija fupi za kugawa zawadi kwa washindi zimeendelea katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania ambapo katika juma lililopita mshindi wa simu ya kisasa wa Dar es Salaam alikabidhia zawadi yake katika maenao ya kimara. Mshindi huyo Bw Erick Mazigo alishukuru kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuwa waaminifu kwa wateja wao na kuwapa zawadi zao.

Promosheni ya winda safari ya Brazil ambayo imekuwa gumzo nchi nzima imeshapata washindi Zaidi ya 100000 wa bia za bure, Zaidi ya washindi 13000 waliojipatia fedha taslimu shilingi 5000 na 10000.

Kunywa kistaarabu; washiriki wanatakiwa kuwa na umri wa Zaidi ya miaka 18; vigezo na masharti kuzingatiwa.
Posted by MROKI On Wednesday, March 26, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo