Meneja
wa kinywaji cha Redd’s Origina Victoria kimaro katikati akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi wa viongozi wa kamati ya Miss Tanzania katika
siku ya kufunga semina ya mawakala wa shindano la Redd’s miss Tanzania
kwa mwaka huu, kushoto kwake ni mkurugenzi wa kampuni ya LINO
Intenational Agency Hashim Lundenga, Redd’s Miss Tz 2013 Happines
Watimanya na Meneja masoko wa TBL Vimal Vaghmaria kulia mwenye miwani.
Redd’s Miss Tz 2013 Happines Watimanya akiwa
katika picha ya pamoja na mawakala wa shindano la Redd’s miss Tanzania
2013 kwenye semina ya mawakala hao kulia waliokaa ni meneja wa Redd’s
Original Victoria kimaro na kushoto ni Meneja masoko wa TBL Vimal
Vaghmaria mwenye miwani na wa mwisho ni mkuu wa itifaki wa kamati ya
Miss Tanzania Albert makoye
======== ======= ======
MAWAKALA
wanaoandaa mashindano ya urembo hapa nchini ‘Redd’s Miss Tanzania 2014”
kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini wametakiwa kutotangaza zawadi kwa
washindi ambazo hawana kwa sababu wakifanya hivyo wanashusha heshima ya
mashindano hayo imeelezwa jana jijini Dar es Salaam.
Akizungmza
jana katika semina ya mawakala hao, Meneja wa bia ya Redd’s Original,
Victoria Kimaro, alisema kuwa hali hiyo inawafanya washiriki, wazazi,
walezi na wadau wa sanaa hiyo kuzungumzia vibaya sanaa hiyo.
Kimaro
aliwataka mawakala hao kuhakikisha wanatangaza zawadi walizokuwa nazo
na kuwakumbusha pia kutafuta warembo wenye vigezo vya juu ili baadaye
mmoja wao aweze kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika fainali za
dunia.
“Usiahidi
kitu usichokuwa nacho, watu wameahidi vitu vikubwa ambavyo
hawajafanikiwa kuvipata mpaka siku ya shindano…sio vizuri na
ninawashauri msifanye tena hivyo ili kujenga shindano letu,” alisema
meneja huyo wa Redd’s.
Aliwataka
mawakala hao pia kufanya mazungumzo na makampuni na taasisi nyingine
kwa ajili ya kuomba udhamini wa kusaidia mashindano hayo na si kutegemea
wadhamini wakuu peke yao ambao wanhitaji kusimamia fainali za taifa
kikamilifu.
“Tujipange
kufanya maandalii yaliyo bora…kama Redd’s tutajaribu kufika kila mahali
kwa uwezo wetu ila nawasisitiza na kuwakumbusha tafuteni mbinu za kuuza
mashindano yenu,” aliongeza Kimaro.
Naye
Mshauri wa Ufundi wa Kamati ya Redd’s Miss Tanzania, Ramesh Shah,
aliwataka mawakala hao kuwaandaa vizuri washiriki kwa sababu wengi wao
wanakuwa ni wahitimu wa elimu ya Sekondari hivyo wanahitaji mwongozo.
Aliwataka
mawakala hao kuthamini sanaa hiyo ya urembo kwa sababu ni moja ya
michezo inayosaidia kukuza uchumi na kutangaza jina la nchi katika ngazi
mbalimbali.
Redd’s
Original ndiyo wadhamini wakuu wa shindano hilo kwa mwaka watatu
mfululizo na mwaka huu wanatarajiwa kutumia zaidi ya Sh. Milioni 500
0 comments:
Post a Comment