Nafasi Ya Matangazo

March 21, 2014

 Rais Kikwete akisisitiza jambo katika hotuba yake
Rais Jakaya Kikwete akilihutubia Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma hii leo wakati wa kulizindua rasmi Bunge hilo la kufaniklisha uandikaji wa Katiba mpya ya Tanzania, huku akisisitiza zaidi katika hotuba yake kwa wajumbe kutumia hekima na busara katika maamuzi yao na kuwaomba kutimiza wajibu wao. 

Aidha pamoja na mambo mengine Rais Kikwete amesisitiza umuhimu wa serikali mbili huku akichambua athari za serikali tatu.

Wengine pichani ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel John Sitta.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma leo
 Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassa Mwinyi na wajumbe wakifuatilia hotuba ya Rais Kikwete leo
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Makungu na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe Amani Abeid Karume na wajumbe wakisikiliza hotuba ya Rais Kikwete leo 
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mhe Tundu Lissu akigonga meza kuashiria kukunwa na hotuba ya Rais Kikwete
 Mjumbe wa Bunge Maalum Mhe Freeman Mbowe akishangilia hotunba ya Rais Kikwete
 Rais Kikwete akihutubia wajumbe wa Bunge Maalum
Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akifurahia jambo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho, na Mhe Mohamed Seif Khatib na wajumbe wengine.
Posted by MROKI On Friday, March 21, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo