Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akizungumza wakati swa hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki mashindano ya NSSF Media Cup yanayotarajiwa kuanza rasmi Machi 29.
Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akizungumza wakati swa hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki mashindano ya NSSF Media Cup yanayotarajiwa kuanza rasmi Machi 29.
Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akimkabidhi vifaa vya michezo, mwakilishi wa timu ya Star Tv, Tom chilala kwa ajili ya mashindano ya NSSF CUP yanayotarajiwa kuanza Machi 29.
Baadhi ya vifaa vilivyotolewa kwa timu shiriki katika michuano ya NSSF Media Cup.
Meneja Kiongozi Idara ya
Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Eunice Chiume (kushoto), akimkabidhi vifaa vya michezo, mwakilishi wa Kampuni
ya Free Media Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Francis
Dande kwa ajili ya mashindano ya NSSF MEDIA CUP yanayotarajiwa kuanza Machi 29.
Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (kushoto), akimkabidhi vifaa vya michezo mwikilishi wa Jambo Leo, Julius Kihampa.
Antony Siame, mwakilishi wa gazeti la Raia Mwema akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (kushoto).
Na Mwandishi Wetu
JUMLA ya sh. millioni 19 zimetolewa na Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), ikiwa ni fedha taslimu zitakazotolewa kwa washindi
mbalimbali wa michezo ya NSSF MEDIA CUP 2014 itakayoanza Machi 29.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja Kiongozi wa Idara ya Uhusiano na
Huduma kwa Wateja wa Shirika hilo, Eunice Chiume, alisema kuwa maandalizi ya michuano hiyo imekamilika na kwa upande wa mpira wa miguu mshindi wa kwanza atapata Tshs.
4,500,000, mshindi wa pili atapata Tshs.3,500,000 na watatu atapata Tshs. 2,000,000.
Aidha alisema, kwa upande wa mpira wa Pete mshindi wa kwanza
atazawadiwaTshs. 4,000,000, mshindi wa pili Tshs.3,500,000 na mshindi wa tatu atazawadiwa
Tshs. 2,000,000 taslimu.
“Wachezaji bora wa mashindano haya kwa upande wa mpira wa miguu na pete wote
wata zawadiwa kila mmoja Tshs 350,000 ili kuongeza hamasa katika michezo hiyo” alisema Chiumea.
Alisema kuwa, mashindano hayo yatashindaniwa kwa njia ya
mtoano kwa mechi za mpira wa miguu na pete, yatashirikisha timu 20 za mpira wa miguu na 18 za mpira
wa pete kutoka vyombo vya habari vya jiji la Dar es Salaam na Zanzibar.
“Timu zitakazoshiriki kwenye mashindano hayo ni IPP, Free Media , BTL, New Habari,
Mwananchi, Uhuru, Habari Zanzibar,
Tumaini Media, Star TV na TBC ambapo kilele cha michuano hiyo iatkuwa tarehe 12
April mwaka huu ambapo mwenyeji wake ni NSSF” alisema.
Alieleza kuwa, mbali ya timu alizozitaja pia kuna timu
nyingine ambazo zipo katika michuano hiyo ikiwa ni TSN, Mlimani, Radio Maria,
Wizara ya Habari, Global Publishers, Jambo Leo,
Raia Mwema na Azam TV ambapo mechi
zote zitafanyika uwanja wa DUCE-Chang’ombe na TCC–Club na fainali kufanyika hapo.
Michuano ya NSSF Media Cup 2014, imetimiza miaka 11 tangu kuanzishwa na inakwenda sambamba na sherehe za miaka 50 ya NSSF na pia mika 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Michuano ya mwaka huu ikifanyika katika sherehe hizo kubwa mbili ndio yenye idadi ya timu zinazoshiriki kuliko mwaka mwingine tangu michuano hiyo ianze mwaka 2004.
Michuano hii ilianzishwa mwaka 2004 kwa kuzishirikisha timu 8 mpaka sasa timu zinazoshiriki zimefikia timu 20 wakati mpira wa Pete timu zimeongezeka kutoka 7, miaka mitano iliyopita tangu mchezo huu ulipozinduliwa kwenye mashindano ya NSSF Media Cup.
0 comments:
Post a Comment