Nafasi Ya Matangazo

March 23, 2014

 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Wilaya ya Moshi Mjini(MNEC) Kamanda wa vijana UVCCM Bw Agrey Marealle Akila kiapo cha utii kwa CCM wakati wa kusimkwa kuwa Kamanda wa vijana wa CCM wilayani humo mbele ya mgeni rasimi Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita(hayuko pichani)
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Wilaya ya Moshi Mjini(MNEC) Bw Agrey Marealle akiwa amekalishwa kwenye kigoda huku akiwa na ngao na mkuki mara baada ya kusimikwa kuwa Kamanda wa vijana UVCCM wilayani humo na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita(hayuko pichani)
Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita(kushoto) akimvalisha kofia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka wilaya ya Moshi Mjini Bw Aggrey Marealle kuwa Kamanda wa Vijana wa CCM wilayani humo Mjini katika halya iliyofanyika viwanja vya CCM katab ya Njoro.
 **************
MJUMBE wa halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi, (CCM), kupitia Moshi Mjini, mkoani Kilimanjaro, Aggrey Marealle, amesema mshikamano miongoni mwa wanachama wa chama hicho ndiyo pekee utakaopelekea chama hicho kufanya vyema katika chaguzi zijazo.
Bw. Marealle aliyasema hayo juzi mjini Moshi, wakati wa hafla ya kusimikwa kwake kama kamanda wa vijana wa umoja wa vijana wa CCM,(UVCCM), wa wilaya ya Moshi Mjini  kwa kipindi cha pili cha miaka mitano, hafla iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa tawi la wakereketwa la Marealle lililopo Kata ya Bondeni, Moshi Mjini.

"Changamoto kubwa ambayo CCM imekuwa ikikumbana nayo nyakati za kuelekea chaguzi mbali mbali ni kutokuwa na mshikamano jambo ambalo mara nyingi hutokana na makundi ndani ya chama, ni vyema tukaepuka hili na msamiati wetu mpya uwe ni mshikamano, hapa tutashinda", alisema.

Aidha alitoa wito kwa wananchi hususan wanachama wa CCM kutokutumia changamoto za kimaisha walizonazo kama sehemu ya maamuzi katika kuchagua viongozi na mstakabali mwingine wa kisiasa.

Katika hafla ya uzinduzi wa tawi hilo la wakereketwa, Bw. Marealle alisema kada ya vijana ni nguzo ya Taifa ambayo haina budi kulindwa kwa kuhakikisha maswala yanayowahusu yanapewa kipaumbele ili wasikate tamaa.

Akihutubia katika hafla hiyo ambayo ilienda sanjari na kusimikwa makamanda wapya wa UVCCM Kata zote za Moshi Mjini, Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mboni Mhita, alisema kuwa kazi kubwa ya makamanda wa vijana wa CCM ni kuwaunganisha vijana, kubaini kero zao na kuzishughulikia kwa wakati.

Bi Mhita alielezea kazi zingine kuwa ni pamoja na kuwasaidia vijana kupata ajira za zikiwemo zile za kujiajiri wenyewe pamoja na kutoa ushauri kwa vijana unaohusiana na mwelekeo wa kisiasa na kimaisha kwa ujumla.

"Kwa kufanya hivi mtakuwa mnaweka nguzo imara ya Taifa kwa ajili ya miaka mingi ijayo", alisema na kutoa wito kwa vijana kuwa tayari kupokea ushauri watakaopata kutoka kwa makamanda hao wapya wa vijana.

Aidha aliwaasa vijana kuiepusha na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na anasa zilizopitiliza ambapo alisema mambo hayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza ari na nguvu kazi ya Taifa.
Posted by MROKI On Sunday, March 23, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo