Nafasi Ya Matangazo

March 19, 2014

 Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo akitangaza washindi wa droo ya sita ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti mara baada ya kuchezesha droo hiyo mapema leo katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.


Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo aeleza jambo kwa wana habari(hawapo pichani)  wakati wa droo ya sita ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti huku akishuhudiwa na Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bakari Maggid(kushoto), Maafisa waandamizi kutoka PWC(wa pili kulia) na push mobile(wa kwanza kulia) mapema leo katika ofisi za Kiwanda cha Bia cha Serengeti jijini Dar es Salaam.
*********
Bia ya Serengeti leo imechezesha droo  yake ya sita ya promosheni ya winda safari ya brazil na Serengeti. Juma lililopita tulishuhudia washindi wakijipatia ving’amuzi pamoja na simu ya kisasa aina ya Samsung galaxy tablet. Wakati huo huo kumekuwa na washindi wengi waliojishindia zawadi za papo hapo kama bia za bure na fedha taslimu . katika droo ya leo wamepatikana washindi wawili wa simu aina ya Samsung galaxy tab.

Droo hiyo ilichezeshwa mapema leo katika kiwanda cha bia cha Serengeti ikishuhudiwa na wanahabari, maofisa kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha, PWC na push mobile media. 

Washindi wawili waliopatikana katika droo ya sita ya winda safari ya Brazil na Serengeti ni Ms. Aquila Machare na Emmanuel Mcharo wote kutoka Majengo katika Manispaa ya Moshi ambao  wamejishindia simu aina ya Samsung galaxy tablet.

Baada ya kupata mshindi wa kwanza meneja wa bia Serengeti Bw Rodney Rugambo aliongea na mshindi huyo aliyekuwa na furaha na alisisitiza kuwa amepata furaha kubwa sana kupata zawadi hiyo. “ hii ni mara yangu ya kwanza kupata zawadi katika michezo ya bahati, sikuwahi kufikiri na mimi nina bahati kiasi hiki na bado sijaamini kama kweli nimeshinda zawadi hii, nawashukuru sana kampuni ya bia ya serengeti kwa kunipatia nafasi hii” alisema Bwana Emmanuel huku akiendelea kuwasisitiza watu kuzidi kushiriki mara nyingi Zaidi.

Pamoja na mvua kubwa na foleni zilizokuwa zikiendelea katika maeneo ya Mbagala wiki iliyopita bado washindi wa ving’amuzi na simu walikabidhiwa zawadi zao katika hafla fupi ya makabidhiano. Mshindi wa simu Bw Mikidadi Omar anayetokea maeneo hayo ya Mbagala alipokea zawadi yake ya Samsung tablet na akatumia muda huo kuwashukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kumpa zawadi hiyo. 

Pamoja nae kulikuwa na washindi wanne wa ving’amuzi ambao ni Bakari Abdallah Jigo kutoka Vingunguti and Rogers Isdory Kuwoko kutoka Tabata,  Alex Sylvester kutoka Zanzibar na Florence Mustapha kutoka Yombo  nao walipewa zawadi zao katika sherehe hiyo.
 
Promosheni ya winda safari ya Brazil na Serengeti kwa sasa ndiyo promosheni kubwa iliyopo sokoni kwa mwaka huu, ambapo kumekuwa na washindi Zaidi ya 100000 waliojishindia bia za bure, washindi Zaidi ya 14,000 waliojishindia fedha taslimu kiasi cha shilingi 5000 na 10000 kupitia kampeni hii.

Meneja wa bia ya Serengeti Bw Rodney Rugambo ameeleza kuwa promosheni hii bado inaendelea na mtu yeyote anayetumia kinywaji cha Serengeti anaweza kujishindia zawadi mbali mbali.

 “ Tunapenda kuwakumbusha wateja wetu kwamba zawadi bado ni nyingi na wazidi kushiriki ili kuzipata zawadi hizo na haswa ile zawadi kubwa ya tiketi ya kwenda Brazil. Pia bado tunazo simu za kisasa pamoja na ving’amuzi vingi, hivyo tunaomba wateja wetu muendelee kunywa bia ya Serengeti kistaarabu huku wakishiriki promosheni yetu maana waweza kuwa mshindi wetu katika droo ijayo.pia tunapenda kuwashukuru wateja wetu kwa kuwa promosheni yetu bado inaenda vizuri” aliendelea Rugambo.

Tafadhali kunywa kistaarabu: kushiriki lazima uwe na umri wa miaka 18 na kuendelea.
Posted by MROKI On Wednesday, March 19, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo